Writen by
sadataley
11:04 AM
-
0
Comments

Rais Jakaya Kikwete
Na Seilla Sezzy, Mwananchi
Mwanza. Rais Jakaya Kikwete ameutaka Uongozi wa Shirika la Umeme (Tanesco) kuimarisha uendeshaji wa shirika hilo ili kuongeza ufanisi katika kazi zake na utoaji huduma za nishati kwa ubora na ufanisi wa juu.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua miradi wa umeme wa Nyakato wenye uwezo wa kuzalisha megawati 60 ambao umegharimu zaidi ya Sh130 billion utakaoingizwa katika gridi ya taifa ili kuondoa tatizo la mgao wa umeme kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Alisema udhaifu wa uongozi wa Shirika la Umeme umekuwa kikwazo cha utoaji huduma bora ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa umeme wa uhakika hivyo kuitaka bodi ya shirika hilo kusaidia uongozi wa Tanesco katika kuhakikisha shirika linakua na kufanya kazi zake kwa ufanisi.
“Tanesco mna matatizo makubwa ya uendeshaji, mnatakiwa kuliangalia jambo hili na kama mnataka kufanya mambo mengine zaidi katika kufanikisha mikakati ya utoaji huduma bora, ni lazima uongozi ushirikiane na bodi, hapa ndipo mtaweza kufanya uamuzi muhimu,” alisema Kikwete.
Alisema shirika linakabiliwa na deni kubwa la kuhakikisha linaboresha huduma zake na uendeshaji ili kwa baadaye Tanesco iwe na kampuni tanzu tatu ndani ya shirika ambazo zitasaidia uendeshaji na kubainisha kampuni hizo kuwa ni kampuni za uzalishi, usafirishaji pamoja na usambazaji.
“Wenzenu wanaozalisha umeme nchi nyingine ndivyo wanavyofanya, Serikali imejenga miundombinu ya umeme kwa gharama kubwa sana lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo,” alieleza.
“Hatuwezi kuwa na maendeleo bila umeme na hiyo ndiyo tofauti ya nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea,” alisema Kikwete.
Chanzo:www.mwananchi.co.tz
No comments
Post a Comment