Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 17, 2013

Mwanamke atoa ushahidi katika kesi ya Ruto ICC

Naibu Rais wa Kenya, William Ruto akiwa ICC hukoThe Hague, September 10, 2013.
Naibu Rais wa Kenya, William Ruto akiwa ICC hukoThe Hague, September 10, 2013.
Shahidi wa kwanza katika kesi inayomkabili Naibu Rais wa Kenya  William Ruto, alisimama Jumanne kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC- iliyoko huko The Hague kutoa ushahidi wake.
Shahidi huyo ambaye hakuonyeshwa sura yake kwa sababu za kiusalama anajulikana kwa namba 536 alikuwa ni mmoja kati ya walionusurika kwenye shambulizi la kuchoma moto lililotokea kwenye kanisa moja la Kiambaa huko Rift Valley baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Bwana Ruto anashtakiwa na mahakama ya ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia ghasia za kikabila zilizotokea nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 1,000 na watu wengine 600,000 walilazimika kukimbia makazi yao na kwenda kuishi katika kambi za muda.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment