Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, September 17, 2013

Benki ya Barclays itasitisha biashara ya kusafirisha fedha Somalia.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza na waandishi wa habari.
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akizungumza na waandishi wa habari.
Benki ya Barclays ya Uingereza.
Benki hiyo ina wasi wasi kwamba kampuni hizo za kusafirisha fedha, zinazofahamika zaidi Somalia kama Hawala zinatumiwa kugharimia ugaidi.

Lakini mashirika ya  huduma za dharura  nchini humo wametoa wito kwa  Barclays kuahirisha mpango wake  ili kuweza kupatikana  mpango mbadala wa kuchukua nafasi ya kampuni hizo ambazo wasomali wengi wanategemea .

Hawala njia ya  kusafirisha fedha kwa simu ni moja wapo ya  biashara kubwa Somalia inayotumiwa na maelfu na maelfu ya wasomali kupeleka na kupokea fedha kutoka nchi.

Barclays iilitishia kufunga akaunti za makampuni hayo mara mbili hapo awali  lakini kubadilisha mpango kutokana na malalamiko makubwa.   Umoja wa mataifa unakadiria kwamba Somalia hupokea dola bilioni 1 na nusu kila mwaka kutokana na fedha zinazopelekwa na  wasomali wanaoishi n’gambo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment