Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, September 5, 2013

Museveni awakutanisha Rais Kikwete na Kagame


Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameitisha mkutano wa dharura wa marais wa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), kujadili hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa waalikwa kwenye mkutano huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Wakati hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikidhoofika, katika siku za karibuni, uhusiano wa Tanzania na Rwanda umekuwa wa shaka hasa baada ya Rais Kikwete kuishauri Serikali ya Rwanda kukaa na wapinzani ili kumaliza mzozo uliolikumba eneo la Maziwa Makuu.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), zilizofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano wa leo utafanyika kwenye Ukumbi wa Commonwealth Resort, Munyonyo katikati ya Jiji la Kampala.
Kwa mujibu wa taarifa Rais Museveni ameitisha mkutano huo hasa kuzungumzia hatua ya Umoja wa Mataifa kupambana na Kundi la Waasi wa M23.
Mbali na viongozi hao wa Tanzania na Rwanda, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo wanatoka Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan, na Zambia.
« PREV
NEXT »

2 comments

  1. Kinachoendelea na ambacho kila mtu anakifahamu ni kwamba Uganda na Rwanda wanavuna kinyebela maliasili ya Kongo.Hawakufurahia hata kidogo kuona Tanzania achilia mbali UN wakiingilia mgogoro huo ili waendelee kuvuna magogo na maliasili nyingine ambazo kimsingi nchi ya kongo kwa ukubwa wake na udhaifu wa jeshi lake na mifumo ya ulinzi wa nchi haiwezi kuzilinda.Ni hili ni jambo la kihistoria ukizingatia muda mwingi nchi imekuwa kwenye mikakati ya vita na kujihami na waasi na wavamizi hasa Rwanda na Uganda wakiwa nyuma ya migongo ya waasi.

    Sasa ni wazi kwa mafanikio ambayo yanapatikana na UN Kongo mashariki,Uganda na Rwanda hawana chao,Musseni hana uhalali wowote kuitisha mkutano huo maana haaminiki na hasa ukaribu wake na Rwanda ambayo UN imekuwa ikisisitiza inawasaidia waasi na kwamba inapora maliasili za Kongo.

    ReplyDelete
  2. Lets hope for good things after the meeting, but honestly mahusiano yetu hasa Tanzania na wenzetu naona kama ni ya kinafiki vile!! Coz licha ya ustaarabu tunaotaka kuusisitiza wenzetu hawako hivyo.... hapa naona kama tunapoteza muda, thus sometimes naona bora ku review mahusiano yetu na majirani zetu then tutengeneze msimamo thabiti kama ambavyo Rwanda wamefanya kuhusu Tanzania. Why not Tanzania against any neighbor? Lusam.

    ReplyDelete