Writen by
sadataley
11:16 AM
-
0
Comments
![]() |
| Ushuhuda unaoishi. |
Gumzo mojawapo katika maazishi ya Askofu Mkuu Moses Kulola, ilikuwa ni mbaba mmoja kumchezea mungu kwa furaha kila linapopigwa pambio ama muimbaji binafsi kupita mbele kwa ajili ya kumsifu Mungu.
Mikononi akiwa na manyanga - manyanga ambayo yameunganishwa na horn speaker, teknolojia ambayo sikuielewa imeendaje endaje kwa haraka haraka. Yalikuwa yakitoa sauti ambayo kwa hakika ilikuwa ni shangwe kwa wanaosikia na kufanyika baraka kwa kila aliyekuwa karibu.
Ndipo Gospel Kitaa kufahamu chanzo cha mzee huyo kuwa bize muda wote kuwa ni kutokana na Yesu alipomtoa, kamtoa mbali sana - kiasi cha kuamua kutomuacha. Baadae ilikuja kufahamika kuwa mtu huyo kumbe ni mchungaji, na katika kuufikia huo uchungaji, kwanza aliponywa ugonjwa mtindio wa ubongo, ama kwa lugha nyingine alikuwa anaumwa kichaa / alikuwa mwendawazimu.
Lakini mara tu alipoombewa na Askofu moses Kulola, mambo yake yalibadilika na sasa kugeukia kumtumikia Mungu na huku akifanyika baraka wa wengine wengi ambao wanapata fursa ya kufahamu kilimchotea.
Sasa sio tena kichaa wala mwendawazimu, amepewa dhamana ya kuongoza watu wa Mungu, kuwageuza kutoka kwenye vifungo vinavyowasumbua na kuwa wavuvi wazuri wa watu. Mchungaji huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, sasa amekuwa mfano. Gospel Kitaa itamtafuta mchungaji huyu na kukuletea habari zake zaidi.

No comments
Post a Comment