Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, September 4, 2013

Bulembo mgeni uzinduzi bodi ya WAZAZI

Na Thomas Mtinge
MWENYEKITI wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bodi mpya ya wadhamini ya jumuia hiyo.
Akizungumza  jana ofisini kwake na mwandishi wa habari hii, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo, Glorious Luoga (Bara), alisema bodi hiyo itazinduliwa leo mkoani Dodoma.
Bodi hiyo mpya inaongozwa na mwenyekiti wake, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba.
Kwa mujibu wa Luoga, uzinduzi huo utafuatiwa na kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Jumuia hiyo Taifa kitakachofanyika kesho mkoani humo.
ìTunaenda Dodoma kwa ajili ya kufanya vikao vyetu vya kawaida kwa ajili ya kupanga mikakati ya kuiimarisha jumuia yetu.
ìWazazi tumejipanga kikamilifu kwa ajili ya kuleta mageuzi ya kiuchumi, kielimu na kisiasa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza wajibu wetu kwa mujibu wa CCM ili kuwaletea maendeleo wananchi wetu,î alisema Luoga.
Pia, aliongeza kuwa kikao hicho cha kamati ya utekelezaji kitafuatiwa na kikao cha makatibu wa mikoa wa jumuia hiyo, ambao mikoa yao ina shule zinazomilikiwa na jumuia hiyo.
ìKikao cha makatibu wa mikoa kitafanyika Jumamosi pamoja na wakuu za sekondari zinazomilikiwa Wazazi.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment