Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, August 15, 2013

Viongozi wa dunia walaani utumaiji nguvu kutawanya waandamanaji Misri

Polisi wanamkamata mfuasi wa rais aliyepinduliwa Misri Mohamed Mursi wakati wa mapambano katikati ya Cairo Ogusati 13, 2013.
Polisi wanamkamata mfuasi wa rais aliyepinduliwa Misri Mohamed Mursi wakati wa mapambano katikati ya Cairo Ogusati 13, 2013.

Viongozi duniani Jumatano wamelaani vikosi vya  usalama vya Misri baada ya kutumia nguvu na kusababisha vifo katika kutawanya wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi.

Marekani pia inalaani vikali ghasia hizo na White House inasema ghasia zitafanya kuwa vigumu zaidi kwa Misri kusonga mbele kwenye njia ya kupata uthabiti na demokrasia ya kudumu.
  • Katika mkutano na waandishi wa habari huko Martha’s Vineyard, Massachusetts ambako rais Obama na familia yake wapo mapumzikoni, naibu msemaji wa rais Josh Earnest alilaani ghasia hizo za Misri.

Alisema Washington inarudia mara kwa mara kutowa wito kwa  jeshi  na vikosi vya  usalama  vya misri kuonesha ustahmilifu na kuheshimu haki za msingi za binadamu kwa raia wa Misri, huku pia wakiwasihi waandamanaji kuandamana kwa amani.

“Pia tunapinga vikali kurudi kwa Utawala wa dharura nchini humo na tunatoa wito kwa serikali kuheshimu haki za msingi za binadamu kama vile uhuru wa mkusanyiko kwa amani na kufuatana na utaratibu unaofuatana na sheria. Dunia inaangalia kile kinachotokea mjini Cairo. Tunaisihi serikali ya Misri na vyama vyote nchini Misri kujiepusha na ghasia na kutatua tofauti zao kwa amani”

Rais Obama hivi sasa anakabiliwa na masuala yale yale  kuhusu namna anavyokabiliana na hali Misri na jinsi anavyokabiliana na kuondolewa madarakani  rais Mohamed Morsi mwezi Julai.

Utawala wa Washington ulikataa kuchukua msimamo kwamba yalifanyika mapinduzi yametokea nchini humo. Chini ya sheria ya Marekani hilo litahitajika kusitisha  msaada wa dola bilioni 1.5 zinazotolewa na Marekani kwa ajili ya uchumi na jeshi la Misri.

Miongoni mwa viongozi walolaani ghasia za jana Cairo ni  Waziri mkuu wa Uturuki recep tayyip Erdogan ambaye chama chake kina ushirika wa karibu na chama cha Muslim Brotherhood, alilaani kile alichokieleza ni  mauaji ya halaiki na kuisihi Umoja wa mataifa kufanya uchunguzi.

Waziri wa mambo ya nje wa uingereza William Hague aliyesema katika taarifa kuwa “ninalaani utumiaji wa nguvu katika kuwatawanya waandamanaji na kutoa wito kwa majeshi ya usalama kuchukua hatua za kujiepusha na ghasia”.

Mataifa ya ulaya pia yalihisihi serikali ya Misri na wapinzani wake chama cha ki-Islam kuepuka kuongezeka kwa ghasia na kurudi kwenye mashauriano ya kisiasa.

Masemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban ki-Moon alisema mkuu wa Umoja wa mataifa analaani ghasia nchii Misri katika maneno makali na anasikitika kwamba  maafisa wa Misri walichagua kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wengi wao wanaharakati wa  ki-islam.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty international lili-litaka jeshi la Misri kuacha kuwashambulia waandamanaji.
Chanzo  www.voaswahili.com/content/viongozi-wa-dunia-walaani-utumiaji-nguvu-misri
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment