Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, August 29, 2013

MSD yapata cheti cha ubora wa kimataifa

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi 
Na Elias Msuya
Bohari ya Dawa Nchini (MSD), juzi ilikabidhiwa cheti cha ithibati cha Shirika la Kimataifa la Viwango (ISO) kutokana na kutoa huduma kwa ubora nchini.
Akikabidhi cheti hicho Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi aliipongeza MSD kwa kuingiakatika mchakato na hatimaye kupata cheti hicho.
“Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza kwa dhati Bohari Kuu ya Dawa, kwa kuingia katika mchakato huu na hatimaye kupata hati ya ithibati,” alisema Dk Mwinyi.
Waziri huyo alisema kumekuwa na wimbi la uingizaji wa bidhaa duni zikiwemo dawa na kwamba nyingine zimeweza kupenya hata katika taasisi za Serikali na kuleta shida kwa wagonjwa wanaotegemea dawa.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani, alisema kutokana na cheti hicho sasa Watanzania watarajie huduma bora za dawa na vifaa tiba.
Alitaja mchakato wa kupata cheti hicho kuwa ni pamoja na kuandaa mpango wa ubora, malengo, viwango vya ubora.
“Tumefanya kazi na TBS na ndiyo wametushauri,” alisema.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment