Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, August 2, 2013

MARAIS WAKOSA MKUTANO

Rais Jakaya Kikwete 
Dar es Salaam. Mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukifanyika Nairobi, Kenya, umemalizika jana bila kuwepo kwa Rais Jakaya Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwakilishwa na Makamu wake, Dk Mohammed Gharib Bilal, huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikisema Rais Kikwete alishindwa kuhudhuria mkutano huo kwa sababu alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra.
Kukosekana kwa viongozi hao katika mkutano huo kumetafsiriwa kuwa kunatokana na mvutano uliopo sasa kuhusu majeshi ya vikosi vya kulinda amani na waasi wa kikundi cha M23 wanaoipinga Serikali ya Congo.
Waasi hao wanadaiwa kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema, “Rais alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand ndiyo maana hakuweza kuhudhuria ila alikuwepo Makamu wa Rais. Hilo la viongozi wa Rwanda na DRC kutokuwepo siwezi kulisemea chochote.”
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi za Maziwa Makuu, walitoa taarifa zao na kujadiliwa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment