Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, August 26, 2013

Kiongozi wa mashirika ya kiraia Kivu kaskazini aomba mkataba wa Addis Ababa uheshimiwe.

Wanajeshi wa Congo wakisubiri kupelekwa kwenye mstari wa mbele wa mapigano huko mashariki ya nchi.
Wanajeshi wa Congo wakisubiri kupelekwa kwenye mstari wa mbele wa mapigano huko mashariki ya nchi.
Kiongozi wa mashirika ya haki za kiraia  huko Kivu Kaskazini Bw.Mustafa Muiti amesema ameshangazwa na ziara ya ujumbe wa maseneta wa Marekani waliokwenda nchini humo kutokuweza kuonana nao na badala yake kukutana na viongozi wa serikali na Monusco pekee.

Akizungumza na Sauti ya Amerika kiongozi huyo ameongeza kwamba ujumbe huo uliokwenda huko mwishoni mwa juma ulikutana na viongozi wa serikali na Monusco  na kufanya nao mazungumzo ambayo walitoa ushauri wa kutafuta  suluhu ya kidiplomasia .

Amesema wazo hilo si baya lakini Congo ilikuwa ya kwanza kufanya mazungumzo,  lakini mazungumzo baina ya viongozi wa DRC na M23 ni kuendelea kushikamana na kubuni njia za kuweza kufikia suluhu ya kudumu ili kuleta amani  katika eneo ambalo limekumbwa na mapigano.

 Kuhusu Marekani amesema angependa  wawaambie Uganda na Rwanda waheshimu mkataba wa Adiss Ababa na pili kuwaambia Rwanda watoke katika ardhi ya Congo wanakowasaidia waasi wa  M23 na pia angependa Rwanda wakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo na kundi la Fdlr  ili waonyeshe  wanakubaliana na diplomasia jambo ambalo litasaidia wale waliokimbia waweze kurudi nyumbani na wao waone amani na usalama kwa maendeleo ya kudumu.
Imewekwa na Happy Adam
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment