Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, July 15, 2013

VITA VINAENDELEA KATI YA WAASI NA WANAJESHI

Vita vikali vinaendelea kati ya wanajeshi, serikali na waasi, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


Wapiganaji (Wanajeshi)
mmoja wa wanajeshi hao amesema kuwa kuwa ndege za kivita za serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku ya kuamkia leo.
Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia mjini Goma.
Mapigano hayo yanatokea, huku jeshi la Umoja wa Mataifa litakalojumuisha wanajeshi elfu tatu likijiandaa kwenda eneo hilo kuwapokonya silaha wapiganaji wa waasi.
Mwaka uliopita waasi hao walijiondoa kutoka mji huo baada ya kuuteka kwa muda.
Mazungumzo ya amani kati ya wasi hao na wawakilishi wa serikali nchini Uganda yamekwama.
Raia wakikimbia makazi yao maeneo ya mashariki ya Kongo
Wakati huo huo, Mashirika ya kutoka misaada ya Kibinadam yamesema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, kukwepa mapigano Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment