Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 27, 2013

Mzindakaya awalipua viongozi

NA MAREGESI PAUL
MWANASIAS A mkongwe nchini, Chrisant Mzindakaya, amesema kama taifa lisipokuwa makini, ipo siku watoto wa kitanzania watakuwa wakifua nguo za ndani za wageni kutoka nje ya nchi. Amesema kwamba, hali hiyo itatokea kwa kuwa viongozi walioko madarakani, wanawajali zaidi wageni kuliko wazawa.

Mzindakaya aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la kujadili changamoto za uongozi na namna ya kuzitatua lililoandaliwa na Taasisi ya UONGOZI.

“Viongozi msiogope kujaribu mambo, viongozi lazima muwe mnathubutu na msiogope kushindwa kwa sababu hata kushindwa ni sehemu ya matokeo.

“Lakini, pia kama tusipokuwa makini, tunaelekea katika kuzalisha taifa la viongozi wavivu pamoja na wananchi wavivu kwa sababu siku hizi kila mmoja ni mwanasiasa.

“Nawaambia, mimi ni mtu mzima, ipo siku watoto wa kitanzania watakuwa wafua chupi za wageni kwa sababu kinachofanywa na viongozi wa sasa ni kuwapendelea wageni na kuwaacha wazawa,” alisema Mzindakaya ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Kwera kupitia CCM.

Kwa mujibu wa Mzindakaya, viongozi walioko madarakani hawawajibiki ipasavyo kwa kuwa hata barua wanazotakiwa kuzijibu kwa wakati, hawazijibu tofauti na enzi za uongozi wa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa akipokea barua na kuzijibu ndani ya wakati.

Kwa upande wake, Rais mstaafu wa Bunge la Afrika, Getrude Mongela ambaye pia aliwahi kuwa Mbunge wa Ukerewe (CCM), aliwapasha mawaziri na kusema baadhi yao hawana kauli nzuri kwa watu wanaowaongoza.

“Jamani samahani sana mawaziri, kuna mawaziri wengine hawana lugha nzuri, sasa kama huna lugha nzuri Rais atakutamaje, lazima kiongozi uwe na lugha nzuri.

“Hata mimi nilipokuwa napigania usawa wa wanawake duniani, nilizunguka dunia nzima na kila niliyekuwa nikizungumza naye, alikuwa akinielewa, nilipokuwa nikizungumza na mchina ananielewa, nikizungumza na nani, ananielewa.

“Tatizo la viongozi wetu wa sasa wengi wao wamechupa, yaani ni kama wamepata uongozi baada ya la mgambo kulia na ndiyo maana siyo wakweli,” alisema Mongela.

Alionyesha kutoridhishwa na tabia ya baadhi ya watu kumtolea Rais lugha zisizofaa kwa kuwa hali hiyo inaonyesha utovu wa nidhamu.

Awali, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema viongozi lazima wawe na mawazo ya kuleta mabadiliko katika jamii na pia wawe wanaheshimika katika jamii.

Chanzo:-www.magazetini.com
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment