Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, July 27, 2013

‘Laana ya gesi yainyemelea Tanzania’

NA KHAMIS MKOTYA, DAR ES SALAAM
SERIKALI imetakiwa kuchukua tahadhari katika uchimbaji wa gesi, kwa ajili ya kuepuka uzembe uliojitokeza katika kusimamia sekta ya madini. Imeelezwa kuwa uchimbaji wa gesi ni fursa nyingine kwa Serikali, kuonyesha umakini katika kusimamia rasilimali za Taifa kwa manufaa ya wananchi tofauti na ilivyo sasa.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la HakiMadini, Amani Mhinda, katika mafunzo ya masuala ya uchimbaji wa mafuta, gesi na madini barani Afrika.

Semina hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Revenue Watch, inahusisha waandishi wa habari kutoka nchi tatu ambazo ni Uganda, Ghana na wenyeji Tanzania.

Akiwasilisha mada yake kuhusu uwazi na uwajibikaji, Mhinda, alisema hatua ya baadhi ya wananchi kupinga usafirishwaji wa gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam, ni matokeo ya hofu ya kubaki masikini.

“Sekta ya mafuta na gesi bado hazijaeleweka vizuri hususani hapa kwetu Tanzania, lakini ni sekta muhimu ambazo zikisimamiwa vizuri zinachangia maendeleo kwa kiasi kikubwa.

“Baada ya kufanya vibaya katika sekta ya madini, hii ni fursa nyingine kwa viongozi wa Serikali ya Tanzania waone ni kwa jinsi gani gesi itakavyowafaidisha wananchi.

“Nionavyo mimi, sekta ya mafuta na gesi ni laana nyingine inayoinyemelea nchi yetu kama Serikali haitakuwa makini, tumepoteza katika madini hatuhitaji kupoteza tena katika gesi,” alisema Mhinda.

Alisema wananchi wamekuwa wakishuhudia fedha nyingi zikitumika katika anasa na matumizi mengine yasiyokuwa ya lazima kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi.

“Mfano wenzetu Botswana, fedha zote za madini zinakwenda katika kuhudumia jamii, wanahakikisha fedha zile zinatumika kwa faida ya wote, lakini sisi hapa kwetu ni tofauti.

“Fedha nyingi zinakwenda katika anasa na ununuzi wa mashangingi, fedha zinazokwenda katika maendeleo ni kidogo kuliko zinazokwenda katika utawala.

“Matumizi ya Serikali yabadilike, kutoka kuhudumia watawala yaende katika kuhudumia wananchi bila kufanya hivyo wengine tutaendelea kubaki watazamaji na wengine wanafaidika,” alisema Mhinda.

Chanzo:-www.mtanzania.co.tz
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment