Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 5, 2013

KODI YA TSH 1000 KWA KILA KADI YA SIMU IMEANZA RASMI

Na Mh. Zitto Kabwe
Kodi ya tshs 1000 kwa mwezi Kwa kila kadi ya simu uliyonayo imeanza rasmi. Bunge la 
wananchi, wawakilishi wa wananchi, limepitisha kodi hii. Hailipwi na kampuni ya simu, inalipwa na Wewe mwenye simu. Kampuni ya simu inakusanya Kwa niaba ya serikali. Ingawa sikuwepo wakati kodi hii inapitishwa na Bunge siwezi kukwepa wajibu wa kuaibika kuwa sehemu ya Bunge hili. Ni aibu Kwa kuwa pendekezo la kodi hii liliondolewa na Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake ya makadirio ya mapato ya Serikali. Pendekezo lilirudishwa namna gani kupitia muswada wa fedha, finance bill, Haieleweki. Ni skandali. Nasikia vibaya sana kuwa mbunge kwenye Bunge lenye maamuzi ya namna hii. Nasikia aibu zaidi kwamba hatukupiga kelele za kutosha kuzuia jambo hili.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment