Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, July 19, 2013

Hali tete kituo cha Ubungo

Na Kelvin Matandiko na Iren Mossi 
Dar es Salaam:Abiria wa Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na idadi ndogo ya huduma za vyoo na vituo vya kupatia chakula.
Mbali na hayo, pia hakuna huduma ya ulinzi wa kutosha kwa abiria kutoka kituo cha Polisi kilichopo hapo,hatua inayozidi kuongeza mwanya wa vitendo vya uhalifu kwa baadhi ya watu wanaoingia na kutoka ndani ya kituo hicho. Hatua hiyo imefuatia baada ya uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kubomoa majengo ya wafanyabiashara mbalimbali waliokuwa wakitoa huduma hizo kwa madai ya kutekeleza agizo la serikali.
Akizungumza na gazeti hili,Katibu wa Kitengo cha Huduma za Barabarani wa Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua),Godwin Ntongeji alisema abiria wameendelea kupata tabu hizo bila kuona juhudi za kufanya maboresho yoyote.
“Kuna mwanamke mmoja hapa hivi karibuni alidondoka,hakukuwa hata na maji karibu,tukaamua kumpeleka chooni kumwagia maji ndio kidogo ikasaidia”alisema Ntongeji.
Akisisitiza changamoto hiyo,Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala Kituo hicho(CMMU),Kimaya Mohamed alisema mamlaka husika wanafahamu lakini hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa.
“Watu wanajisaidia maeneo ya wazi hali ambayo inaashiria wazi kuwa hakuna hata ustaarabu usalama wa mali za abiria ni kidogo sana,kila siku tunahangaika sana majira ya usiku kwani huwezi kujua yupi ni abiria na yupi ni kibaka”alisema Mohamed.
Akijibu madai hayo jana,Msemaji wa Halmashauri Jiji la Dar es Salaam,Gaston Makwembe alisema kuhusu suala la huduma ya vyoo vinne vilipo vinatosha na kwamba suala la usalama lipo mikononi mwa kituo cha polisi kilichopo hapo.
“Si hivyo tu kuna ulinzi shirikishi wanatoa ushirikiano wa kutosha pale, kwa hivyo tunategemea kesi zote za kiusalama zitakuwa zinafanyiwa kazi na kituo hicho,”alisema Makwembe.
Makwembe aliongeza kuwa changamoto ya usafi na huduma ya vituo vya chakula mpaka sasa wanaendelea kuifanyia kazi.
“Kuna vibanda vya muda ambavyo vitafunguliwa kuanzia leo, kwa ajili ya kufanyia biashara ya chakula na suala la usafi kuna mtu mwenye zabuni ya kufanya usafi hapo Ubungo ambaye tutazungumza naye kumaliza suala hilo,”alisema Makwembe.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment