Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, June 21, 2013

Uchaguzi wa udiwani Arusha sasa Juni 30

Dar es Salaam.Tume ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kurudiwa kwa uchaguzi mdogo katika kata nne za Arusha ambazo ni Kimandolu, Elerai, Themi na Kaloleni ambazo zilisimamishwa kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa madiwani kutokana na vurugu zilizojitokeza katika kampeni za mwisho za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na sasa utafanyika Juni 30 mwaka huu.
Mkurugenzi wa NEC,Julius Malaba alisema jana Dar es Salaam kuwa kutokana na hali hiyo, wananchi wa eneo hilo wanapaswa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura,ili waweze kuhakiki majina yao ili kuondoa usumbufu siku ya kupiga kura.Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo wananchi wa eneo hilo wametakiwa kutulia kwenye makazi yao mpaka uchaguzi utakapofanyika tena.
Malaba alisema ikiwa NEC imetangaza kusimamisha uchaguzi katika maeneo yoyote nchini, wanasiasa wanapaswa kuacha kufanya kampeni mpaka uchaguzi utakaporudiwa tena, na kwamba ikiwa baadhi ya vyama vitabainika kwenda kinyume na sheria hiyo vitafikishwa kwenye kamati ya maadili kwa sababu watakuwa wamevunja sheria za uchaguzi.
Alisema, kutokana na hali hiyo,wananchi wanapaswa kuwa makini katika kipindi hiki na kuhakikisha kuwa hawashiriki kwenye mikutano ya kampeni inayofanyika maeneo yao ili kuondoa migogoro ambayo inaweza kujitokeza.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment