Writen by
sadataley
4:16 PM
-
0
Comments
KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA
DAYOSISI YA IRINGA
"NAFASI YA KIJANA KATIKA KANISA".
SOMO LILOTOLEWA KATIKA KONGAMANO LA VIJANA KATIKA USHARIKA WA KIHESA 29-06-2013
Kanisa ni nini?
Kanisa si jengo tu bali ni wale waliomo ndani yake. Maana yake ya asili toka neno la Kiyunani ni ekklesia “kusanyiko” "walioitwa" kama maneno katika msalaba ambao huwa ninauvaa. Neno Kanisa Iimo katika Biblia, Matendo ya mitume 17:24 "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono."
Kanisa si jengo tu bali ni wale waliomo ndani yake. Maana yake ya asili toka neno la Kiyunani ni ekklesia “kusanyiko” "walioitwa" kama maneno katika msalaba ambao huwa ninauvaa. Neno Kanisa Iimo katika Biblia, Matendo ya mitume 17:24 "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono."
Kanisa ni watu wanao amini Waefeso
2:21 "Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe
hekalu takatifu katika bwana." 1Wakorintho 3:16 "Hamjui ya kuwa ninyi
mmekuwa hekalu la Mungu na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?.
Kazi ya kanisa ni ipi? Kanisa linaeneza
ijili 2 Timotheo 4:2 "Lihubiri neno
uwe tayari wakati ufaao na wakati usiokufaa karipia kemea na kuonya kwa
uvumilivu wote na mafundisho."
Kanisa limepewa maagizo na Mungu
Waefeso 4:12 "Kwa kusudi kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma
itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe."
Kila mshiriki ana jukumu maalum 1
Wakorintho 12:13, "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa
mwili mmoja kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani ikawa tu watumwa au ukawa
tu huru nasi tulinyweshwa Roho mmoja."
Wakristo tu wafariji wenzetu Waebrania
10:25 "Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine;
bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa
inakaribia.
Hivyo naenda kusema kuwa ndiyo sababu siku zote nikijitazama
kama kijana humuona Mungu kuwa ni wa ajabu kuniumba hata mimi na kunifanya kuwa
Mchungaji. Hivyo hukubaliana na nyimbo na waimbaji hawa ambao wamewahi sema
kupitia nyimbo zao kuwa
a.
“Mungu wetu ndiye Boma”- Tumwabudu Mungu Wetu 302 na Dr. Martin
Luther
Mungu ndiye ngao yetu na siraha yetu shetani akija kwetu tukiwa
naye daima tutashinda na maadui zetu (shida,adha na changamoto za maisha
yetu yote). Tumtazame yeye kama Dr.
Martin Luther alivyosema katika maneno ya wimbo wake huu. Anaimba wakati akiwa
katikati ya mapambano na sisi tuimbe tunapopita katika hali mbalimbali katika
maisha yetu.
b.
“Mungu ni Mwaminifu”. -Solomon Mkubwa
Mungu hatotuacha daima yeye hutunza maagano(makubaliano yetu
nay eye) hivyo hata sisi tulivyo hapa anatujua na anaendelea kutunza uaminifu
wake kwetu hivyo na sisi tusimame kwake tu, tumtazame yeye pekee.
c.
“Liseme kwani ni jambo usilolijua”- Sarah K
kwani ni hakika hatuna tunalolijua katika
maisha yetu ni yeye (Yesu) anatuwezesha ,ametuwezesha na ataendelea kutuwezesha.
d.
“I will be There, Just Call My
name”. -Michael
Jackson&Mariah Carey
Ipo siku tutaitwa kwenda Mbinguni na kila mmoja wetu ataitwa
kwa jina lake; hivyo tujiandae.
e.
“Heri Kumjua Yesu Bwana”. Tumwabudu Mungu Wetu 175 na F.J Crosby
Ni Yesu pekee atatuwezesha na kutuvusha na hata sasa anajua
tulikotoka,tulipo na tuendako.
f.
“Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana”.
Tumwabudu Mungu Wetu 268 na samuel Stone
Kama tulivyoimba siku ile ya Kipaimara hebu tuendele
kumtazama yesu kama msingi wa Kanisa na ndiyo njia pekee ya kutuvusha vijana,
njooni tumtumikie kadili ya nafasi tunazojali. Tusiogope huku ni kuzuri tu
hakuna shida yoyote.
LEO HII NAKUONA KIJANA MWENZANGU KAMA:-
- MSHARIKA
MKAMILIFU ALIYEPO NA AJAYE
- KIONGOZI
WA KANISA-MZEE WA KANISA-MTUMISHI WA MUNGU KADA MBALIMBALI
- MLEZI
WA FAMILIA AJAYE NA ALIYEPO (wajibu wako pale nyumbani kwa sasa).
- MZAZI AJAYE – (unayoyafanya sasa nawe utafanyiwa na m/watoto wako).
- MTETEZI
WA WANYONGE (Haki za wanyonge na
wanaonyanyaswa kuto kaa kimya kwani Dr. Martin Luther alisema utawajibika
kwa yale uliyoyasema na usiyoyasema lakini ulipaswa kuyasema na umekaa
kimya.)
- MWANA
MAENDELEO ( Jiandae kuajili au
kuleta mabadiliko katika eneo ambalo Mungu atakupa/amekupa).
A. “Mkumbuke Muumba wako siku za
ujana wako kabla hazijaja siku zilizo mbaya…” (Mhubiri12:1)
B. “Nimewaandikia ninyi vijana, kwa sababu mna nguvu,
na neno la Mungu linakaa ndani yenu,
nanyi mmemshinda yule mwovu”.
(I Yohana 2:14b).
C. “Na nimwibie mpenzi wangu wimbo wa mpenzi wangu
katika habari za shamba lake la mzabibu. Mpenzi wangu alikuwa na shamba la
mizabibu,kilimani penye kuzaa sana;akafanya handaki kulizunguka pande zote,
akatwaa mawe yake,akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, akajenga mnara
katikati yake, akachimba shinikizo ndani yake;akatumaini ya kuwa utazaa zabibu,
nao ukazaa zabibu-mwitu. Na sasa, enyi wenyeji wa yerusalem, namyi watu wa Yuda
amueni, nawasihi mkato, kati ya mimi na shamba
langu la mizabibu….”(Isaya 5:1-7).
UELEWA JUU YA UJANA NA KIJANA
1.
Ujana
ni hatua ambayo mtu anaipitia baada ya utoto au ni kipindi cha kati cha makuzi
ya mtu kabla ya utu uzima na hatimae uzee
2.
Ujana
huanza mara baada ya mtu kubadilika kimaubile na huanzia miaka kumi na mbili
wengine hadi kumi na tano ambapo mtu huanza kuwa na hisia za kimwili na
kutamani sana kuwa na uhuru wake katika maamuzi. Mabadiliko haya huchochea au
hupelekea hisia mbalimbali za kimwili na mabadiliko ya jumla ya tabia
3.
Ujana
ni majira yanayopita katika makuzi ya mwanadu, ukifanikiwa kuwa mzee ni lazima
ulipita katika kipindi hiki au daraja hili la ujana, kwa hiyo kama bado uko
katika dara hili ni muhimu kujipanga ili usije ukajilaumu mbele ya safari
ZINGATIA HII
“Huwezi kuyajali maisha yako kama
hujui thamani yake, huwezi kujua thamani ya maisha yako kama hujajitambua kwa
Neno la Mungu, huwezi kuwa na maisha ya mafanikio kama maamuzi yako
hayatengenezi mafanikio, ufahamu sahihi juu ya maisha yako ndio msingi wa
kujitambua kwako, yaani kuijua Kweli ili hiyo Kweli ikuweke huru na ndipo
utakapokuwa huru kweli kweli, kumbuka hata usipoamua maisha yako yataendelea
kama kawaida. Zaidi ya hayo kama hujui wewe ni nani huwezi kujua thamani yako,
kama hujui thamani yako lazima utaishi chini ya kiwango cha maisha unayotakiwa
kuishi”.
UTAIJUAJE NAFASI YAKO KAMA KIJANA
Nafasi yako kama Kijana ni wajibu
wako, umuhimu ulionao kwako na kwa jamii kwa ujumla wake pamoja na familia
yako. Lazima ujue nafasi yako katika maeneo yafuatayo:
• Kwako binafsi,
• Katika familia yako,
• Kwa Kanisa lako,
• Kwa jamii yako
• kwa mkoa wako,
• kwa Taifa lako na
• kwa Ufalme wa Mungu.
Safari ya kujua nafasi yako katika
maeneo yako hayo hayo hapo juu inaanzia katika eneo moja tu ambalo ni KUJITAMBUA
KUJITAMBUA NI NINI
“Kujitambua ni hali ya kuwa na
ufahamu au uelewa (kujua) wa kutosha juu ya maisha yako kwa ujumla pamoja na
mazingira yanayokuzunguka na hivyo kukufanya uishi maisha yanayofanana au
kulingana na kusudi la Mungu kwako, uishi katika ubora wa maisha yanayolingana
na kiwango cha ufahamu ulionao au kiwango cha kujitambua kwako kutegemeana na
nguvu ya taarifa unazopata.
HIVYO BASI KIJANA ANATAKIWA
KUJUA KUWA:-
1. Kujitambua ni hatua ya muhimu
katika maisha ya mtu yoyote duniani kama anataka kuishi kwa Furaha na matumaini
na kufikia malengo yake
2. Kujitambua ni matokeo ya kupata
ufahamu sahihi juu eneo fulani utakaokusaidia kufanya maamuzi sahihi katika
eneo husika ili uweze kufanikiwa
3. Ufahamu au maarifa unapatikana
kwa kutafuta, kuchunguza na kudadisi taarifa mbalimbali kwani si kila namna ya
kujitambua ni sahihi kwa kijana
4. Matokeo ya ufahamu ulionao
yatafanana na ubora wa maisha unayoishi kwa kiwango cha kuathiri maamuzi yako
ya kila siku
5. Kiwango cha matokeo ya kujitambua
kitafanana na ubora wa taarifa ulizozipata
6. Udhihirisho wa maisha ya
kujitambau ni hatua ya juu kabisa ya kuthibitisha kwamba kweli umejitambua.
KUJITAMBUA NI LAZIMA KWANI:-
1. Ni lazima ujitambue, upate
ufahamu sahihi juu ya maisha yako pamoja na mambo yote na jamii inayokuzunguka
2. Ni muhimu ujue wajibu ulionao
kwako wewe mwenyewe kama mtu binafsi juu ya maisha yako
3. Kuna haja ya kujua kuwa wewe ni
sehemu ya familia yako na lazima ujue wajibu wako kwa wazazi na familia kwa
ujumla
4. Ni lazima ujifunze kuwa mzalendo
wa taifa lako sawa na jinsi ambavyo Mungu anataka, fahamu kuwa umeunganishwa na
ardhi ya Tanzania kwa mafanikio yako, Mungu akikwambia nenda nje ya nchi nenda
lakini usifikiri mafanikio hayako Tanzania
5. Kijana unatakiwa ujitambue, ujielewe kuwa wewe ni nani na una kusudi gani katika maisha yako
6. Unatakiwa kupata uelewa wa
kutosha juu ya kipindi cha ujana na umuhimu wake ukiwa bado Kijana ili ujue
namna ya kuzingatia na kujipanga kwa hapo baadae
7. Kuelewa changamoto zilizopo
katika kipindi cha ujana na namna ya kuzishinda kuna uhusiano na namna
unavyojitambua ukiwa bado kijana
8. Kujenga shauku, nia na kiu kwa
kijana ili aweze kuishi maisha yenye mwelekeo na aweze kutimiza maono yake
akiwasaidia na wengine kumjua Mungu na maisha yake kwa ujumla wake
9. Kuwekeza uthamani na nguvu ya
kipindi cha ujana kwa mtazamo wa Ufalme wa Mungu.
Imeandaliwa na
Mchg Kurwa Sadataley- Mratibu wa
Idara
Habari na Mawasiliano KKKT-DIRA
No comments
Post a Comment