Writen by
sadataley
8:50 PM
-
0
Comments
Mchungaji: Polisi mkiwapiga risasi na Mabomu hawa wengine watazaliwa!!
Mkuu wa jimbo la Arusha Magharibi na Mchungaji wa Kanisa la KKKT,Mchg Kisiri amesema kuwa anasikitika kwa Kifo cha Judith Moshi kilichokatizwa na watu alie waita Wanyama na Magaidi kwa kurusha Bomu ktk mkutano wa CDM.Alisema kwamba Amani na utulivu tulionayo ipo mashakani kutoweka kwa ajili ya viongozi wanaoshindwa kusoma Alama za Nyakati huku wakiendeleza Porojo na Hadithi badala ya kujibu kero za wananchi.na wamekua wakitumia Risasi na mabomu kuwatisha wana nchi.
Aliwaambia wanausharika na wasio washarika kuwa wasife Moyo na wasiogope maana Mungu yupo upande wao. Na kwamba polisi kutumia risasi na mabomu kuwaua sio suluhisho kwani wakiuwawa hawa wengine watainuka.
Aliyasema hayo kataka ibada ya Mazishi ya Marehemu Judith Moshi.
No comments
Post a Comment