Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Tuesday, June 25, 2013

BW. NAYMAN CHAVALLA: "HATUWEZI KUMALIZA TATIZO LA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA"

Bw. Nayman Chavalla Katibu Mkuu KKKT Dayosisi ya Iringa

 Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa KKKT,Dayosisi ya Iringa alipokuwa akizungumza na wageni marafiki wa kituo cha kulea watoto walio katika  mazingira hatarishi( magumu) cha Huruma. Wageni hao wametoka  Usharika wa Kilutheri  Carvaly nchini Marekani,ambapo wamekuwa na mahusiano na kituo hicho tangu mwaka 1998. Kituo hicho   ni maarufu kwa jina la Huruma Center ( Huruma Diaconical center) kinachomilikiwa na KKKT Dayosisi ya Iringa.

Pia  Bw. Nayman Chavalla  amewashukuru kwa kuendelea kukisaidia kituo na kuwaomba waendelee kufanya hivyo kwani kwa kufanya hivyo wanachangia katika kuubadilisha ulimwengu na kusaidia katika kuendeza juhudi za Kanisa katika kumsaidia mtu kamili yaani kiroho na kimwili.

 Aidha amesema kituo cha Huruma kimebahatika kuwa na marafiki wa uhakika ambao ni Berlin Mission na Usharika wa  Carvaly Lutheran toka Marekani. Na hakusita kusema pia wakati mwingine hupokea misaada mbalimbali toka St. Paul  na sharika mbalimbali ili kuchangia huduma mbalimbali zinazohitajika katika kituo hicho.

                                              
                                                 Mama Constancia Chilewa  Msimamizi wa Kituo

                                                                     
                                Profesa Gabriel K. Nzalayamisi   Mwenyeji Mkazi wa Wageni   
                                           
                                    Mchungaji Sara Wirth   toka Usharika wa Carvaly Lutherani Marekani




Katibu Mkuu akiwaelekeza juu ya mradi wa miti katika kitalu cha miti kilichopo makao makuu ya Dayosisi


                       Hapa wakiwa katika ofisi ya Waandishi wa redio Furaha 96.7 FM
    Meneja wa Redio Furaha Bw. Protasi Kanemela akitoa maelezo huku Katibu Mkuu pembeni akimsikiliza kwa umakini mkubwa
   Hapa wakiwa sehemu ya majadiliano

                                       Hapa wakiwa katika Studio ya Redio Furaha
Watangazaji Noel Kaguo na Shukuru Mgoba wakiwa katika kipindi cha Nyota ya Asubuhi
   Mtangazaji  Noel Kaguo



« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment