Writen by
sadataley
1:27 PM
-
0
Comments
Mama tunakushukuru sana kwa mapenzi mema ni maneo ya Baba askofu Dkt. O.M Mdegella wa K.K.K.T-Dayosisi ya Iringa
"Hongeara mama" ni maneno ya Mchungaji Sara Mdegella kwa mama Ann Katrinn Person
Hii ni zawadi yako Mungu akubariki sana
Ubarikiwe sana
Nashukuru sana ni maneo ya mama Mchungaji Runne Persson
Tunakutakia maisha mema na Mungu akipenda tutaonana
IFUATAYO NI SEHEMU YA HOTUBA YAKE
Ninawashukuruni sana! Kwanza ninashukuru kwa jioni hii njema kwa ninyi nyote
mliofika kwa kuniaga taja…, ni neema
ya pekee. Ninashukuru mno! Halafu ninataka kusema asante kwa moyo na upendo mmenionyesha
wakati nimekuwepo hapa Iringa, DIRA. Wengine nimekaa nao sana, na wengine
tumeonana kwa kifupi tu. Lakini ninataka kusema kwamba ukaribu wenu pamoja na
ukarimu umenitia moyo sana na imenisaidia kujisikia kama nipo nyumbani
hapa, asanteni sana.
Wenzangu wa
ETE, Mchg. Vallence, Mchg. Sarah, Mchg. Ulime na Mary, kama mimi ninavyoona
tumefanya kazi vizuri pamoja. Tumepanga kazi,
tumezungumza, tumecheka na tumeomba pamoja ili kazi ya ETE isonge mbele
na watu wapate nafasi kumfahamu Mungu wetu anayetaka watu wote wamfahamu Yesu Kristo katika maisha yake.
Pia ninasema asante Sarah,
kwa muda huu tuliokuwa pamoja ofisini na kwenye safari zetu za kuzunguka
majimboni kuwaona wenzi wa wachg. na wainj. Umekuwa tayari kunieleza mambo yote
ambayo sikuelewa na sikufahamu, na umekuwa tayari kunijibu kila swali. Hii
imekuwa msaada mkubwa kwangu na imenisaidia sana katika kazi yangu. Sasa naomba
Mungu akubariki katika kazi ya kuchunga Usharika wako, wenzi wa wachungaji na
wainjilisti.
Miaka hii
michache nimejifunza mengi kutoka kwenu. Na kitu kikubwa hasa ni maana ya maisha ya maombi.
Ninaporudi
nyumbani nitaendelea kutoa habari za kazi ya wenzi katika usharika wetu
ili wafadhili wenu wapate changamoto kuendelea kujitolea kwa kupitia SEM.
Muda umeenda
haraka, miaka 2 ½ imeshapita, na sasa livu yangu imekwisha na
nimeitwa kazini nyumbani tena. Mwakani Mungu akipenda, ninataka kufika hapa
tena kumtembelea Rune na ninyi nyote, nafikiri Mungu anapenda.
Mungu awabariki ninyi nyote na tutaendelea kuwa pamoja katika maombi,
asanteni sana!
No comments
Post a Comment