Writen by
sadataley
2:42 PM
-
0
Comments
WAZIRI MSTAAFU MH. FEDRICK T.SUMAYE AWAFUNDA WASOMI CHUO KIKUU IRINGA (THE IRINGA UNIVERSITY) ZAMANI TUMAINI UNIVERSITY-IRINGA JUU YA UZALENDO AONYA VITA ZA KIDINI KUTIKISA TAIFA
HAYO AMEYASEMA ALIPOKUWA AKIONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA CHUO KIKUU HICHO . AMBAPO JUMLA YA SHILINGI MILIONI 116,807,650 ZILIPATIKANA IKIWA SHILINGI MILIONI 22,557,650 FEDHA TASLIMU NA AHADI IKIWA NI SHILINGI MILIONI 94,250,000
pichani Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fedrick T.Sumaye na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma wakishiriki ibada kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Moses Mdegella na Msaidizi wake
Mchungaji Blastone Gavile wakiongoza ibada kabla ya kuanza kwa harambee hiyo
Mkuu wa chuo hicho akimuongoza mgeni rasmi katika ofisi yake tayari kwa kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza harambee hiyo
Katibu Mkuu Bw. Nayman Chavalla akifurahia jambo na Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye
Waziri Mkuu Mstaafu akisaini kitabu cha wageni
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Moses Mdegella akikazia jambo kama sehemu ya maandalizi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo
Mkuu wa Chuo cha iringa Profesa Nicholaus Bangu akimuongoza Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fedrick T.Sumaye kuelekea kwenye mti aliopanda katika chuo hicho kama kumbukumbu yake mwaka 2002
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Moses Mdegella akiteta jambo na Katibu mkuu wa Dayosisi Bw. nayman Chavalla
Huu ndiyo mti uliopandwa na Mh. Waziri Mkuu Mstaafu mwaka 2002
Viongozi waandamizi wa Dayosisi , Chuo wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi mbele ya mti huo
Mchungaji Msigwa Mbunge wa Iringa Mjini akitoa salam zake katika harambee hiyo
Mkuu wa Chuo cha iringa Profesa Nicholaus Bangu akitoa hotuba katika harambee hiyo
Waandishi wa habari wakiwa katika kazi kulia ni Dada Tukuswiga Mwandishi wa Redio Furaha 96.7fm Fm
Kwaya Kuu ya K.K.K.T-Dayosisi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kwa umakini mkubwa
Waziri Mkuu Mstaafu akisaini kitabu cha wageni
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Moses Mdegella ,Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fedrick T.Sumaye na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma wakiwa katika harambee hiyo
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye akizungumza na wasomi wa chuo cha Iringa
Mbunge Msigwa (kulia)akizungumza na msaidizi wa Askofu Dean Blastone Gavile
wa K.K.K.T Dayosisi ya Iringa
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa chuo cha Iringa ambako mgeni rasimi ni Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye
Mbunge Msigwa akisalimia katika harambee iliyoendeshwa na Sumaye leo katika chuo cha Iringa
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amewafunda wasomi wa chuo kikuu Iringa zamani Tumaini kuwa watumie kanisa hilo litakalojengwa kwa ajili ya kueneza amani zaidi huku akiwataka kuachana na masikitiko yasiyo kwisha yanayotokana na baadhi yao kutojituma katika kazi.
Sumaye ametoa kauli hiyo leo katika hotuba yake kwa wasomi wa chuo kikuu cha Iringa kabla ya kuanza kuendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la chuo hicho.
Amesema kuwa katika Bibilia rushwa na ufisadi ni dhambi kubwa katika Taifa na kuwa vitu hivyo tunavilea wenyewe japo kuna tatizo kubwa na kuwa kaburi pekee la mambo machafu ni ujenzi wa kanisa hilo na matumizi yake kutumika kwa malengo ya kuhubiri amani na kukemea ufisadi.
" Mfano ni nani kati yenu amepata kutozwa rushwa na mkulima ila rushwa inatozwa na wenye nafasi na hivyo lazima vijana wasomi mkumaliza hapa lazima kwenda kubadilisha Taifa....ndio maana nilipoitwa na baba askofu kwa ajili ya changizo la kanisa nikasema nitafika kwani ni jambo jema"
Sumaye alisema kuwa kumshangilia mtu anayeendesha gari la kifahari kwa kulipata kwa njia ya wizi ni hatari na kuendelea kuliangamiza Kanisani.
Alisema kuwa hivi leo watu wanajenga chuki kati ya wanyonge na matajiri na kuwa hivi sasa limezuka jambo baya zaidi kwa watu kuchukiana kwa misingi ya dini zao na kuwa nchi yeyote itakayoingia katika machafuko ya imani ni hatari zaidi.
Sumaye alisema kuwa vita ya kiimani ni mbaya zaidi na siku zote vita hiyo huwa haina mshindi hivyo ni vema kila dini kuanza utaratibu wa kuwafundisha vijana wake ili kuwa na uzalendo katika Taifa hili.
Aidha alisema kuwa mapambano ya dini yanayoendelea mbali ya kutokuwa na mshindi ila bado vita hiyo haitakuwa na mshindi na hivyo ni vema kila mmoja kuachwa akiendelea kuamini kile ambacho ana amini hata kama ni chini ya mti asisumbuliwe.
Alisema vita ya udini inayoendelea kwa sasa ni mbaya zaidi na kuwa watanzania tusiruhusu vita hiyo kupandikizwa .
Pia alisema kuwa hivi sasa wapo baadhi ya watu wanaendelea kuharibu Taifa hili wakiwemo baadhi ya watu wanaoharibu miundo mbinu ya barabara kwa kung'oa vyuma chakavu.
Waziri Sumaye alisema kuwa anafurahishwa zaidi kuona nyumba za ibada zinaendelea kujengwa na hivyo ni imani yake nyumba za ibada zitasaidia kuhubiri amani na utulivu pamoja na uzalendo miongoni mwa watanzania.
No comments
Post a Comment