Writen by
sadataley
10:42 AM
-
0
Comments
ASKOFU MPYA KKKT SHINYANGA ASIMIKWA, KANISA JIPYA LAZINDULIWA
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Gharib Bilal ameshuhudia kuapishwa na kuingizwa rasmi kazini kwa mchungaji Emanuel Joseph Makala katika kazi ya uaskofu kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania dayosisi ya Kusini Mashariki mwa ziwa Victoria, mkoani Shinyanga kazi iliyoongozwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Dkt. Alex Gehaz Malasusa pamoja na maaskofu wengine wa kanisa hilo mapema hii leo.
Ibada hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mkoani hapo pia imeshuhudiwa tendo la uzinduzi wa kanisa jipya la dayosisi hiyo akiwemo waziri mkuu mstaafu mheshimiwa Edward Lowassa pamoja na wageni mbalimbali wa kanisa hilo na ndugu jamaa na marafiki waliokuja kushuhudia tendo la kuapishwa kwa askofu Makala.
![]() |
| Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Alex Gehaz Malasusa. |
![]() |
| Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria ibada hiyo. |
![]() |
| Askofu Malasusa akiongoza kubariki kiti kitakachokuwa kikikaliwa na askofu wa dayosisi hiyo. |
![]() |
| Muonekano wa kiti baada ya kubarikiwa |
![]() |
| Mchungaji Makala akiwa mbele tayari kubarikiwa. |
![]() |
| Maaskofu wakiwa wamemzunguka mchungaji Makala wakati tendo la kumbariki likiendelea. |
![]() |
| Mchungaji Makala baada ya kubarikiwa na kukabidhiwa nyenzo za kazi mkononi. |
![]() |
| Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akiwa kanisani asubuhi ya leo. |
![]() |
| Baadhi ya waimbaji na wapigaji waliokuwepo kanisani hapo. |
![]() |
| Kwaya ikimsifu Mungu kanisani hapo. |
![]() |
| Waziri mkuu mstaafu mheshimiwa Edward Lowassa mkono wa kushoto akiwa ibadani. |
![]() |
| Baadhi ya umati wa watu ukiwa umekaa nje baada ya kukosa viti ndani. |
![]() |
Picha na habari kwa hisani ya bundalawilliam.blogspot.com |


















No comments
Post a Comment