Writen by
sadataley
9:45 AM
-
0
Comments
MAUAJI YA PADRE ZANZIBAR


Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu
Katoliki Tanzania (TEC),Severin Niwemugizi alisema tukio hilo linatia mashaka
kwa kuwa mauaji hayo yanaonyesha kuwa ni ya kupanga.
“Nimepata taarifa kwamba kuna mwenzetu ameuawa huko,
lakini inaonekana ni mauaji ya kupangwa kwa kadiri ya hamasa ambazo zinatolewa
na dini fulani, kwani waliwahi kusema hatutaifurahia Pasaka, nadhani ndiyo
wanatekeleza hilo,” alisema Niwemugizi.
Alisema tukio hilo ni la kuogopesha na
linaonyesha nchi inakoelekea si kuzuri kwa kuwa kikundi fulani kimeachiwa na
kinafanya mauaji na kuwatendea maovu wengine lakini viongozi wamekaa kimya.
“Hii ni ishara mbaya kwani Serikali
ipo hivyo tunahitaji kauli yao kuhusu haya mambo, kwa kweli nina mashaka na
yanayotokea ili yasije yakatufikisha kwenye mauaji ya kimbari yaliyotokea
Rwanda,”alisema Niwemugizi.
JK atuma rambirambi
Rais Jakaya Kikwete alisema amepokea
kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Mushi.
“Nimeliagiza Jeshi la Polisi nchini
kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa
kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na
kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
Picha na habari kwa hisani ya angazakimataifa.blogspot
No comments
Post a Comment