Writen by
sadataley
9:34 AM
-
0
Comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya jana, Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na waumini wa Dayosisi ya Kaskazini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuuaga mwili wa Askofu wa Jimbo hilo, Askofu Dkt. Thomas Laizer.
Rais Kikwete na ujumbe wake amewasili kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha kiasi cha saa 10:50 akaenda moja kwa moja kuaga mwili wa Marehemu Laizer na baadaye akakuta na kuwafariji wafiwa akiwamo Mke wa Askofu Laizer, Mama Maria Laizer.
Rais pia atashiriki mazishi yake yaliyopangwa kufanyika kesho, Ijumaa, Februari 15, 2013 katika Kanisa Kuu hilo la KKKT la mjini Arusha.
Askofu Dkt. Thomas Olmorijoi Laizer ambaye alizaliwa Machi 10, mwaka 1945 katika Kijiji cha Engarenaibor, Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha alifariki dunia Alhamisi iliyopita, Februari 7, majita ya saa 12 jioni kwa magonjwa ya Kisukari na Shinikizo la Damu.
Habari kwa hisani ya Mjengwa Blog
Picha kwa hisani ya bashir-nkoromo.blogspot.com
JK AONGOZA MAELFU MAZISHI YA ASKOFU MSARIKIE
RAIS Jakaya Kikwete, jana aliongoza maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, mkoani Kilimanjaro, wananchi na wageni kutoka ndani na nje ya nchi, katika mazishi ya aliyekuwa Askofu mstaafu wa kanisa hilo jimbo la Moshi, Amedius Msarikie (82).
Mazishi hayo yalifanyika katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme, mjini humo ambapo katika salamu zake, Rais Kikwete alisema marehemu alipenda maendeleo, kusimama na kushiriki kwa vitendo katika mambo mbalimbali ambayo aliyaamini.
“Askofu Msarikie alianzisha Chuo Kikuu kinachotoa mafunzo
kwa walimu wa sayansi eneo ambalo Serikali inahitaji kubwa,
hii ni kazi nzuri ambayo haina budi kuigwa na kuendelezwa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, Serikali itaendeleza
juhudi zote alizoanzisha ili kuchochea maendeleo zaidi.
Alisema marehemu alikuwa muumini mkubwa wa amani, upendo
na mshauri mzuri katika mambo mbalimbali ambayo yatamfanya aendelee kukumbukwa siku hadi siku.
Rais akiweka shada la mauaMazishi hayo yalifanyika katika Kanisa Kuu la Kristu Mfalme, mjini humo ambapo katika salamu zake, Rais Kikwete alisema marehemu alipenda maendeleo, kusimama na kushiriki kwa vitendo katika mambo mbalimbali ambayo aliyaamini.
“Askofu Msarikie alianzisha Chuo Kikuu kinachotoa mafunzo
kwa walimu wa sayansi eneo ambalo Serikali inahitaji kubwa,
hii ni kazi nzuri ambayo haina budi kuigwa na kuendelezwa,” alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa, Serikali itaendeleza
juhudi zote alizoanzisha ili kuchochea maendeleo zaidi.
Alisema marehemu alikuwa muumini mkubwa wa amani, upendo
na mshauri mzuri katika mambo mbalimbali ambayo yatamfanya aendelee kukumbukwa siku hadi siku.
Rais akiweka mchanga katika kaburi la Askofu
Picha zote kwa hisani ya kajunason.blog

No comments
Post a Comment