Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 8, 2018

Ousmane Dembele ataka kuondoka Barcelona


Nyota wa klabu ya FC. Barcelona, Ousmane Dembele, amesema hana furaha na taarifa zinazoeleza kuwa Kocha wake, Ernasto Valverde, ana mipango ya kumsajili mchezaji Antoine Griezmann kutoka Atlerico de Madrid.

Dembele amesema kama Valverde atamsajili mchezaji huyo, basi ataondoka klabuni hapo na kwenda kucheza soka sehemu nyingine.

Kauli hiyo imekuja kufuatia tetesi ambazo zimeanza muda mrefu kuwa Barcelona inataka kumsajili Mfaransa huyo, ambaye amekuwa tegemeo kubwa ndani ya Atletico Madrid.

Ikumbukwe Dembele alijiunga na wakatalunya hao msimu uliopita wa majira ya joto akitokea Borussia Dortmund kuja kuchukua nafasi ya Neymar Jr aliyeuzwa kwenda PSG ya Ufaransa kwa kiasi cha pauni milioni 200.

Ujio wa Dembele ndani ya Barcelona ulikuwa ni kuchukua nafasi ya Neymar, japo alipatwa na majeruhi mapema tu baada ya kujiunga na timu, lakini ujio wa Coutinho mwezi January uliondoa pengo lake kwa kikosi kuimarika.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment