Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 8, 2018

Arsenal kuibuka na ushindi leo?


Arsenal inadhamiria kuepuka msururu wa matokeo ya kushindwa mfululizo watakapocheza na AC Milan mechi ya mkondo wa kwanza hatua ya 16 bora ya michuano ya ligi ya Europa siku ya Alhamisi.

Arsenal imepoteza michezo minne mfululizo ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwezi October 2002.

Arsenal itacheza bila Hector Bellerin, Nacho Monreal na Alexandre Lacazette kutokana na majeraha halikadhalika Pierre-Emerick Aubaneyang atakasokena.

AC Milan, inayoongozwa na Gennaro Gattuso imefanya vizuri kwenye mechi 13 bila kufungwa

Inashikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ya Serie A, ikiwa na alama 25 nyuma ya Napoli, lakini kiungo wa kati wa zamani wa Rangers, Gattuso, aliyechukua nafasi ya Vincenzo Montella aliyetimuliwa mwezi Novemba, ameubadilisha msimu wao.

Katika mechi yao ya mwisho waliichapa Lazio 5-4 kwa mikwaju ya penati na kuingia fainali ya Coppa Italia na hawakuwahi kuruhusu goli katika mechi zake sita zilizopita.

Kwa upande mwingine, matokeo mabaya ya Arsenal yamewafanya kuwa nafasi ya sita katika msimamo wa ligi kuu Uingereza, alama 13 nyuma ya Tottenham iliyo nafasi ya nne.

Kuhusu michuano ya Europa league Wenger anasema ''hii ni fursa ambayo lazima tuitumie, inaongeza msukumo zaidi ''.

''ni ngumu ukiwa unapitia kipindi kigumu, lakini ni fursa nzuri kuonyesha una ubora na nguvu na unaweza kuonyesha hilo panapokuwa na ugumu.

''ni fursa nzuri kuonyesha tunaweza kulikabili na kwa kipindi kijacho itafanya kikosi kuwa na nguvu zaidi.

Hata hivyo, kwa sasa ushabiki kutoka kwa wapenzi wa Wenger umeshuka , 88% ya chama cha mashabiki wa Arsenal,AST mashabiki 1000 walipiga kura jumatatu wakitaka mkataba wa Wenger uvunjwe mwishoni mwa msimu.

Msemaji wa chama hicho anasema ''matokeo ya utafiti wetu yanaonyesha Arsene anaheshimika, lakini kumekuwa na maoni kuwa haipeleki Arsenal mbele''.

''Ujumbe wetu kwa klabu ni kuwa wachukue hatua haraka bila kuchelewa''.

'Arsenal ina wachezaji wazuri'

Arsenal imeshinda mechi nne kati ya 15 walizocheza na hawajawahi kupoteza mechi tano tangu mwaka 1977 walipopigwa kwenye michezo minane mfululizo kuanzia tarehe 12 February mpaka tarehe 12 March.

Pamoja na Gunners kupambana, Gattuso anasema anatarajia kuwa na mchezo mgumu huko San Siro.

Alisema:''Arsenal haiko kwenye wakati mzuri,lakini ina wachezaji wazuri na wamefunga magoli 18 kwenye ligi hii ya Europa.Tunawaheshimu sana na lazima watoe matokeo mazuri.

''tumekuwa vizuri kiakili,kiufundi,na kimbinu lakini hatuwezi kufanya makosa,hatutaogopa mashabiki 70,000 ambao watakuwa San Siro , tutaonyesha ubora wetu kwa ufundi, lazima tuipe ugumu Arsenal.

''Timu za Italia zinafanya vizuri Ulaya, hata hivyo hatuwezi kufananisha Mpira wa Uingereza na Italia siku hizi.Miaka kumi iliyopita ilikuwa kinyume, lakini leo wachezaji walio juu huenda kwenye ligi kuu ya Uingereza.

« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment