Writen by
sadataley
7:08 PM
-
0
Comments
SIKU
YA CCT (JUMUIYA YA KIKRISTO TANZANIA
CHUO KIKUU DAR ES SALAAM
MAHUBIRI
YA 25.01.2015
ZABURI
133
Leo ni siku ya CCT Jumuia ya
Makanisa Tanzania leo imetimiza miaka 81, lilianzishwa 25/01/1934 likiwa na
lengo la kuboreshwa kuanzisha shughuli nyingine zinazojibu mahitaji ya watu.
Hivyo tupo kusherehekea kazi na utume ambao wenzetu walikaa na kuona kuna haja
ya kukaa na kushirikiana pamoja kwa sisi tulio katika mwamvuli mmoja.(Waprotestant).
Kwa sasa mwenyekiti wake ni
Askofu Dr. Alex Gehaz Malasusa na Katibu
Mkuu ni Mchungaji Dr. Leonard Mtaita.
Jumuiya hii ina tunu zake (core value za
CCT) –Love (upendo), Compassion (matendo ya huruma), Unity(Umoja) and
Ecumenism, Professionalism (Utaalam), Faithfulness (Ukweli), Transparency
(Uwazi), Accountability (Uwajibikaji), Stewardship (Utoaji),
Trustworthy(Uaminifu) ,Integrity(Uwezo) na Honesty
Wanachama wake ni (CCTchurch members)Evangelical Lutheran Church in Tanzania(ELCT),Anglican
Church Tanzania(ACT),Moravian Church of Tanzania(MCT),Africa Inland Church
Tanzania (AICT),Mennonite Church in Tanzania (MCT),Baptist Church in Tanzania
(BCT),Salvation Army,Presbyterian of East Africa (PEA),Bible Church Tanzania,
African Brotherhood Church,Church of God in Tanzania na Evangelistic Church of
Mbalizi.
Vyama
vilivyopo chini ya CCT ni Bible Society of Tanzania, Tanganyika Refugees
Service, Youth Men’s Christian Association ,Young Women’s Christian
Association, Africa Enterprise Evangelistic ,Life Ministry, Mission Aviation
Fellowship, Emmanuel International, Summer Institute of Linguistic, Dodoma
Christian Medical Center, Mennonite Central Committee na Compassion
International Tanzania
Makanisa
yaliyo chini ya CCT (Chaplaincy)umoja huo ni Chuo Kikuu Dar es Salaam (UD),
Mzumbe, Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) na Chuo Cha Kilimo Morogoro(SUA).
Wayahudi waliamini kuwa Yerusalem ilikuwa ni kila kitu,
huu ni mji wenye milima mingi sana na ndipo
palipojengwa hekalu. Palikuwa ni
mlimani hivyo ilikuwa ni sehemu ya juu kabisa. Na katika Hekalu kazi yao kubwa ilikuwa ni kwenda kuabudu tu.
Mlima Herimoni upo Kaskazini
ya Yerusalemu, inayoonekana juu ya Yordani, kulikuwana mvua kubwa sana na
barafu.Maji yake hutiririka hadi Yeriko. Wayahudi leo hii wanaimba wimbo huu ili
kuonyesha furaha kubwa kwani walikuwa na
uhakika wa kukutana na Mungu wao.
Zaburi hii inawapa Tumaini na
Baraka kwa wote waliomtegemea na inafungua mlango wa Imani na Baraka hasa
ikizingatiwa kuwa hekalu lilikuwa juu kabisa na kupelekea wao kuamini ndiyo
Injili ilipoanza kutawanyika. Bwana
anaandaa familia ya waaminio. Umoja huleta vionjo na unyevu uliopo katika mlima
huu ni kama Roho Mtakatifu amebeba utakaso wa Wana wa Mungu. Na hii inatokana
na ukweli uliopo kuwa hakuna anayeweza kupima upendo wa kimahusiano uliopo kati ya Mungu na watoto wake.
Ili maisha yawe bora na yenye
furaha ni lazima upendo uwepo. Imani si
lazima uone kwa macho moja kwa moja
kilichopo ni kukubali tu; Heri wale ambao wanamuamini lakini hawajauona.
Ni kama vile Yesu anavyomwaambia Tomaso katika Yohana 20:29.
Ni ndipo tunachokiona kuwa
Injili inatawanyika na kutengeneza familia ya Kikristo. Na leo tuna mamilioni
ya Wakristo na kumwamini Yesu Kristo katika Umoja, Tumaini, na Upendo. Upendo
ni mbegu na zaburi hii imejikita sana katika kuyaweka pamoja makabila ya
Israel. Na haiishii hapo inafika na katika familia zetu, jamii zetu na Kanisa.
(2 Korintho 13:11, Waefeso 4:1-6, Wafilipi 2:2-8 na wakolosai 3:14-15).
Jambo kubwa tunaloliona katika
Zaburi hii ni umoja katika Baba [Mungu] anayejidhihirisha kwetu kwa njia ya
Yesu Kristo. Ndugu [kaka-kindred] “Brother” si kwa ajili ya ndugu wa damu
lakini ni kwa ajili ya wale wanaounganishwa na Neema ya Mungu. Na jambo kubwa
hapa ni sisi ni kumwabudu Mungu na kuwaleta wengine kwa Yesu kwa njia ya
Uinjilishaji.
Hivyo na sisi leo tuone kama
tupo kwa ajili ya imani hiyo na kuwafanya wengine wamwanini Mungu na kuuona umoja ambao ulianzishwa na Yesu. Hasa
wale waliopo katika mabonde[dhambi, wahitaji walioonewa,wasiopata haki za msingi].
Tunaona mafuta yakitumika kama
kimiminika kinachoweza kutelemka. Na kuona ubarikio[ ordination] wa Aaron
Walawi 8:12. Hivyo wale wote
waliobarikiwa wamewekewa mafuta ya Aaron juu yao. Kwetu sisi mafuta ni ishara
ya kuabudu[worship],kufunga[feast],sherehe ndani ya Ushirika na Mungu.
Ujio wa Yesu kwetu sisi ni
kuja kutupa maji sisi tulio na kiu ,Yesu amekuja kwa ajili ya wale wasio na
chakula, malezi, haki na upendo wapate yote hayo Yesu anatupenda sote. Yesu
asingalikuja tungekuwaje.
Yesu amekuja kutupa Tumaini
yeye amekuja kwa ajili yetu. Sisi ni wanae tu, familia moja ya Kikristo ya
waaminio. Umoja wa hapa duniani ndiyo utakao tupeleka Mbinguni.
Tunapoelekea
katika uchaguzi Mkuu
Nchi yetu iko katika njia
panda inaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo na hali ya maisha ya wananchi
wote kuboreka kutokana na ugunduzi wa gesi asilia, kuendelea kupanuka na
kuboreka kwa huduma za kijamii, kupanuka
kwa sekta binafsi na fursa nyingi za biashara, jitihada kubwa za ujenzi wa
miundombinu na mambo mengine mazuri yaliyofanywa na serikali za awamu zote.
Ipo hatari ya taifa letu
kupasuka kutokana na dalili za mpasuko wa kidini, mmomonyoko wa maadili kwenye
jamii, kuporomoka kwa imani ya wananchi kwa dola ufa katika muungano na
umaskini na tofauti kubwa ya kipato baina ya watu na hali ya kukata tama
miongoni mwa wananchi. Uongozi madhubuti, uongozi wa zama za sasa unahitajika.
Rais ajaye ana kazi kubwa
zaidi ya kusimamia umoja wanchi yetu na usalama, amani na utulivu kuliko
viongozi waliopita. Lazima kiongozi ajae ayajue kwa kina mazingira ya sasa, awe
ameyaishi, na kutambua mahitaji yake.
Nchi yetu ni kubwa sana na ina
takribani makabila 120 makubwa na madogo ina ukubwa wa ardhi wa kilomita za
mraba laki tisa na nusu, ni muungano wan chi mbili; nusu ya wananchi wake
wakiwa wamezaliwa ndani ya uongozi wa Rais Mkapa na Kikwete na vijana chini ya
miaka 35 ni asilimia karibu 80, na wengi wao wakiwa hawana ajira.
Kuna viashiria vya nyufa kati
ya wakulima na wafugaji,wachimba madini wadogo na wawekezaji wakubwa, Wakristo
na waislamu, wabara na wazanzibari, matajiri na maskini wa kutupwa.Rais wa
Awamu ya Tano awe ni mtu mwenye kuzitambua changamoto hizo na kuwa na mkakati
wa kuzitatua.
Inategemea wajihi yaani character, wa kiongozi mwenyewe.
Hivyo, wajihi wa mgombea unapaswa kujibu maswali yanayoletwa na changamoto
hizi.Tumeshuhudia miji ikikua kwa kasi kubwa na umaskini ukiongezeka mijini
hali iliyozaa uhalifu na uvunjifu wa amani.
Tunae soma tusome kwa bidii na
tusitegemee sana kuajiliwa tuanze kutafuta na kuziona fursa. Tupo hapa chuo
Kikuu kwa sababu ya Baraka na upendo wa Mungu. Tupo hapa kwa kusudi la Mungu
tu. Yesu awe rafiki yetu siku zote.
Ni dhahiri kwamba tofauti ya
kipato baina ya walionacho na wasionacho imeongezeka. Hivyo tunaposherehekea na
kuadhimisha sikuu hii tuombe roho ya umoja iwe kwetu ili amani, upendo na
uvumilivu tuliokuwa nao tuendelee kuwa nao daima. Siku ile ya mwisho tutakuwa
kundi moja na mchunga mmoja. (Mahali ni Pazuri 244 na TMB324),hivyo tuishi kwa kupendana na kusaidiana.
Ameni
Imeandaliwa na
MCHUNGAJI KURWA SADATALEY
VITABU
REJEA
MacDonald
William Believers Bible Commentary
Adeyemo
Tokunboh The African Bible Commentary: A one Volume Commentary written by 70
Africa Scholars
New
Interpreters Bible vol. VI (Nashvile Abingdom, 1996)
James
Limburg, Psalms (Louisville, KY: Westmister John Knox, 2000)
Richard
Clifford, Psalms 1-72 (Nashivile: Abingdon, 2002).
Paul J. Achtemeier, ed. Harper Collins Bible Dictionary (HarperSanFrancisco, 1996), 41
Paul J. Achtemeier, ed. Harper Collins Bible Dictionary (HarperSanFrancisco, 1996), 41
No comments
Post a Comment