Writen by
sadataley
2:28 PM
-
0
Comments
Rais wa Venezuela amemtaja Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa kama saratani na kikaragosi cha Marekani.
Zeid Ra’ad al-Hussein, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa
Nicolas Maduro aliyasema hayo jana Ijumaa katika hotuba iliyorushwa mubashara kwenye runinga ya taifa na kuongeza kuwa, Zeid Ra’ad al-Hussein, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa hana haki ya kukosoa namna nchi hiyo ya Amerika ya Latini inavyoongozwa.
Matamshi ya Maduro ni radimali baada ya afisa huyo wa ngazi za juu wa UN kusema kuwa haki za binadamu zinakiukwa nchini Venezuela, mbali na vyombo vya dola kukandamiza taasisi za kidemokrasia.
Rais Maduro amesema, "Kamishna Mkuu ni mtumwa wa mafashisti walio dhidi ya haki za Wavenezuela na kibaraka wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ambaye anasambaa kama saratani katika mfumo wa haki za binadamu. Ni mtu ambaye amepoteza itibari na asiye na hadhi ya kutoa maoni yoyote kuhusu nchi yetu."
Zeid Ra’ad al-Hussein, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa hivi karibuni alisema amepokea mamia ya ripoti kuhusu mauaji dhidi ya waandamanaji, yaliyofanywa na maafisa usalama katika miaka ya hivi karibuni nchini Venezuela.
Parstoday
No comments
Post a Comment