Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, March 10, 2018

Rais wa Mauritius kujiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi

Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Jugnauth amefichua kuwa rais wa nchi hiyo Ameenah Gurib-Fakim yupo katika ncha ya kujiuzulu kutokana na kashfa ya ufisadi inayomuandama.
Port Louis, mji mkuu wa kisiwa cha Mauritius
Jugnauth aliyasema hayo jana Ijumaa huko Port Louis, mji mkuu wa kisiwa hicho kilichoko katika bahari ya Hindi na kubainisha kuwa, sakata la ufisadi wa kifedha linalomsakama rais huyo limemsukuma ukutani na hana chaguo jingine ila kujiuzulu.
Amesema, na hapa tunanukuu, "Tumekubaliana na rais kuhusiana na yeye kujiuzulu na hata tarehe ya kuachia ngazi." Hata hivyo Waziri Mkuu huyo wa Mauritius alikataa kuwaambia waandishi wa habari kuhusu tarehe ya kujiuzulu rais.
Vyanzo vya habari nchini humo vimefichua kuwa rais huyo atajiuzulu rasmi Jumatatu ijayo ya Machi 12, baada ya nchi hiyo kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.
Ameenah Gurib-Fakim, ambaye ndiye rais mwanamke pekee kwa sasa barani Afrika, anatuhumiwa kuchota fedha kutoka kwenye akaunti ya Asasi Isiyokuwa ya Kiserikali ya Planet Earth Institute yenye makao yake London Uingereza, na kutumia fedha hizo katika masuala ya kibinafsi.
Gurib-Fakim mwenye umri wa miaka 58 amekuwa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya kisiwa hicho, tokea mwaka 2015.
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment