Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, March 4, 2018

Kigwangala: Shughuli za kibinadamu zinachangia uharibifu wa maliasili


Waziri Wa Mali Asili Na Utalii Dk. Hamis Kigwangala amesema Shughuli Za Kibinadamu Zinachangia Kwa Kiasi Kikubwa Kuharibu Mali Asili Za Taifa.

Dkt Kigwangala alisema Hayo Wakati Akifunga Mafunzo Maalumu  Ya Utunzaji Wa Mali Asili Katika Taasisi Ya Taaluma Ya Wanyamapori Iliyopo Pasiansi Na Kusema Shughuli Za Kibinadamu Kama Vile Kilimo Na Uchimbaji Madini Usio Zingatia Utaratibu zimekuwa zikichangia uharibifu huo.

Kigwangala Amewataka Wahitimu Hao wanapaswa Kutumia Mbinu Walizojifunza Katika  Ili Kuzuia Uharibifu Wa Mazingira Usitokee Na Kupunguza Nguvu Kubwa Inayotumiwa Na Serikali Kufanya Doria Na Ukaguzi Barabarani Wakati Tayari Misitu Imeharibika.

"Ninaomba wahitimu mtumie mbinu mlizopata na mtumie njia ya teknolojia na mawasiliano ya kisasa zaidi ili mzuie uharibu wa misitu kwa njia ya kisasa zaidi kwani inaokoa gharama za doria, alisema.

Awali Akitoa Taarifa Ya Taasisi Hiyo Mbele Ya Waziri wa Mali Asili Na Utalii  Mkuu Wa Tasisi Hiyo Bi.Lawael Damalu Alisema jumla ya wanafunzi 64 walijiandikisha lakini 62 ndiyo wamehitimu na  wawili wakishindwa kuhitimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo ujauzito.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment