Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, March 1, 2017

Facebook yafuta michoro ya utupu


Blackman na bintiye Christabel mwaka 2005

Facebook imezuia duka moja la michoro nchini Australia kuchapisha michoro ya utupu.
Michoro hiyo ya Charles Blackman inayojulikana kama Women Lovers, inaonyesha wanawake wawili walio uchi ambao wako kitandani kando mwa paka.

Muuza michoro Mossgreen, alijaribu kuutangaza mchoro huo kupitia kwa Facebook lakini mtandao huo uliukataa.

Mkurugenzi mkuu wa Mossgreen Paul Summer, anaitaja hatua hiyo ya Facebook kama ya kushangaza.

Facebook inasema kuwa uamuzi wake ndio wa mwisho lakini Mossgreen wameichapisha tena michoro hiyo.

Mwezi uiopita mwalimu mmoja nchini Ufaransa aliushtaki mtandao wa Facebook, kwa kufuta ukurasa wake baada ya kuchapisha picha ya utupu ya mwanamke iliyochorwa karne ya 19.

Bwana Summer anasema mchoro huo wa Women Lovers, ulitarajiwa kuuzwa kwa zaidi ya dola 34,000 wiki ijayo. 
Chanzo:Muungwana Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment