Writen by
sadataley
6:37 AM
-
0
Comments
Cristina Scussia akifanya yake jukwaani, picha ndogo jaji amebaki akiduwaa asiamini aliyepo jukwaani©The Voice Italy/YouTube. |
Mtawa huyo mchangamfu pia kwa muonekano anaonekana anaweza fani ya uchekeshaji aliweza kuimba kwa ustadi kiasi cha kuwasimamisha mashabiki ukumbini humo, hata majaji walipokuwa wakigeuka kuangalia nani anaimba hawakuamini macho yao kumuona mtawa huyo, huku pia msafara wa watawa wenzake waliomsindikiza wakiwa chumba maalumu cha watangazaji walikuwa wakirukaruka juu kwa furaha.
Akiulizwa maswali baada ya kumaliza kuimba kuwa ni kwanini ameenda kwenye The Voice, mtawa huyo akajibu anakipaji ambacho anatakiwa kukitumia kwao, au hakitakiwi kutumika hapo? jibu ambalo lilipokelewa kwa makofi ya shangwe kutoka kwa majaji na watazamaji. Swali lililofuata ndilo ambalo GK inadhani mtawa huyu pia fani ya kina Joti anaiweza ni pale alipoulizwa je uwepo wake katika shindano hilo baba mtakatifu Papa Francis anajua? kwa sauti ya uchangamfu na kujiamini Cristina akajibu "Kwakweli sijui, ila nasubiria papa anipigie simu, huwa kila siku anatuhimiza twende nje tukahubiri, kumjua Mungu hakutuondolei vipaji tulivyonavyo bali tunapata zaidi na ndio maana nipo mahali hapa", alisema Cristina jibu ambalo lilipokelewa kwa nderemo ukumbini hapo.
Tukio la mtawa Cristina ni la kipekee kwakuwa amewakilisha vyema wenzake ambao wana vipaji kama hivyo lakini hawavionyeshi wakiogopa mazingira yaliyowazunguka, yeye ndoto yake toka akiwa mtoto ilikuwa ni uimbaji, hata shirika la watawa analofanyika kazi walipoandaa tamasha la muziki ndiko alikojigundua kipaji hicho na sasa amekianika wazi. Ukweli ni kwamba kuna wengi wenye vipaji kama mtawa huyo lakini hawajajivua gamba, wakivua gamba kuna kitu cha mabadiliko kitatokea. The Voice ni shindano maarufu barani Ulaya lilianzia nchini Uholanzi mwaka 2011 kabla nchi nyingine hazijaomba ridhaa ya kuandaa mashindano hayo ambayo yamekuwa yakichukua umaarufu kukaribia mashindano mengine ya uimbaji kama X Factor, Idols, Got Talents.
No comments
Post a Comment