Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, March 24, 2014

MAUAJI KANISANI MOMBASA KENYA WAKATI WA IBADA LEO



Watu wawili mwanaume na mwanamke wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya watu wasiofahamika wakiwa na bunduki walifyatua risasi ndani ya kanisa la Joy in Jesus maeneo ya Likoni karibu na mji wa bandari ya Mombasa nchini kenya wakati wa ibada jumapili ya leo.

Kwa mujibu wa afisa polisi wa mji wa Likoni Robert Mureithi amesema mtu huyo akiwa na bunduki alifyatua risasi ovyo kanisani humo kisha kukimbia, ambapo majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu ingawa haijaelezwa wamejeruhiwa kiasi gani. Mpaka sasa haijajulikana waliyehusika na tukio hilo ingawa kutokana na mashambulio ya mfululizo, kuna uwezekano wa kundi la Alshabaab kuhusika na shambulio hilo.

Ingawa pia katika mji wa Mombasa kumekuwa na tabia ya waumini wa dini ya kiislamu wenye imani kali kutotaka wakristo wawepo katika mji huo ikiwa pamoja na mji wa Mombasa kujiondoa kwenye jamhuri ya Kenya.Kwa mujibu wa kamanda Mureithi amesema mpaka sasa usalama umeimarishwa katika eneo hilo na jeshi hilo limeanza uchunguzi kubaini waliohusika na shambulio hilo.

Ni hivi majuzi polisi mjini Mombasa waliwakamata watu wawili wakiwa ndani ya gari na mabomu waliyoyatengeneza ndani ya gari hilo ikielezwa kwamba mabomu hayo yalikuwa na uwezo wa kuharibu majengo makubwa. Tayari tahadhari imetolewa nchini humo kuhusiana na matukio hayo ambayo yanaweza kusababisha maafa makubwa nchini humo, hivyo watu wametakiwa kuwa waangalifu.

MUENDELEZO

Mpaka sasa ni jumla ya watu wanne wameripotiwa kufariki dunia na wengine 17 wamejeruhiwa vibaya baada ya tukio hilo ambalo limeacha majonzi na simanzi nchini Kenya.

SAMAHANI PICHA ZIFUATAZO NI MBAYA

Damu zikiwa zimetapakaa kanisani.
Mmoja wa majeruhi akipata matibabu hospitalini © standarddigital news
Mbunge Abdullswamad Shariff Nassir akimpa pole mmoja wa majeruhi anayepatiwa matibabu hospitalini. ©dailynation
Habari na Gospel Kitaa
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment