Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, November 1, 2013

BARAZA LA MAKANISA KENYA LAUNGA MKONO VIONGOZI WA MAKANISA KUKABIDHIWA BUNDUKI KUJILINDA

Katibu mkuu wa Baraza la makanisa nchini Kenya NCCK mchungaji Peter Karanja. ©Dailynation.
Watu mbalimbali nchini Kenya wakiwemo waumini wa dini ya Kikristo wamepinga wazo lililotolewa na viongozi wa dini hiyo kwamba wakabidhiwe bunduki aina ya AK47 ili kupambana na waumini bandia wa dini ya kiislam nchini humo ambao wamesababisha kifo cha mchungaji pamoja na kuchoma kanisa huko mkoani Mombasa nchini Kenya.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kupitia mitandao ya kijamii watu hao wametaka serikali kutokubali maombi yao badala yake wazidishiwe ulinzi majumbani pamoja na sehemu zao za ibada. Akizungumza  huko Kaloleni Mombasa wakati wa maziko ya mchungaji Charles Mathole wa RCG aliyeuwawa kwa kupigwa risasi kanisani mijini Mombasa, mchungaji Lambart Mbela wa kanisa hilo aliiomba serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenza wake William Ruto kuwakabidhi wachungaji na viongozi wa dini ya kikristo silaha aina ya AK47 ili kupambana na waislamu bandia wanaoharibu hali ya hewa nchini humo.

"Wachungaji, maaskofu na viongozi wote wa Mombasa tumeona sasa yatosha kuendelea kunyanyasika na hali hii kutoka kwa waumini bandia wa kiislamu ambao wanaua wachungaji wakati wa maandamano, wanachoma moto makanisa, hebu serikali tupeni haki ya kumiliki AK47 kwakila mchungaji, askofu na viongozi wa kanisa ili kupambana na waumini hawa bandia, kwa kujilinda, kuwalinda waumini wetu na makanisa yetu na mali zetu maana maisha ya wachungaji yapo hatarini, sasa tunaomba tukabidhini tuwafundishe kazi kwamba kanisa ninani". amesema mchungaji Lambart Mbela

Wakati huohuo baraza la makanisa nchini Kenya NCCK tofauti na matarajio ya wengi, limeunga mkono ombi la viongozi wa dini hiyo mjini Mombasa yakukabidhiwa silaha hiyo kutokana na viongozi hao kuona silaha hiyo itakuwa muafaka kwa ulinzi wa maisha yao, waumini na mali zao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment