Writen by
sadataley
8:53 PM
-
0
Comments
Wakuu wa Niger wamewakamata wahamiaji zaidi ya 100 wakielekea Algeria.
Wanasema watu hao wanazuwiliwa na polisi.Hatua hiyo inafuatia vifo vya watu zaidi ya 90, wakiwemo wanawake na watoto, ambao walikufa kutokana na kiu wakati wakivuka jangwa la Sahara.
Serikali ya Niger piya imetangaza kuwa itafunga kambi zote za wahamiaji kaskazini mwa nchi, ambazo hazitambuliwi.
Katika taarifa yake iliyosomwa kwenye televisheni serikali pia ilisema kuwa wale wote wanaoshiriki katika biashara ya kuwasafirisha wahamiaji kimagendo, kwa kupitia Niger Kaskazini hadi Algeria na Libya, watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali.
Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Niger, Mohamed Ba-zoum, ameiambia BBC kuwa mji wa Agadez peke yake, kaskazini mwa Niger, una wahamiaji kama elfu tano kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kwenye kambi zisizoruhusiwa.
No comments
Post a Comment