Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, November 1, 2013

HUENDA HUYU NDIYE PAPA MTOTO AJAYE, AKETI MAHALA HUSIKA

Mtoto ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiwa amemkubatia Papa, ambaye alikuwa akifundisha. Picha kwa hisani ya L'Osservatore Romano kupitia AP.

Mtoto mmoja alijikuta mwenye bahati ya pekee jijini Roma, wakati alipopanda kukifikia kiti cha kiongozi wa kanisa katolkiki duniani, Papa Francis, na kuketi – jambo lililowafanya wengi kupigwa na butwaa mwishoni wa wiki iliyopita.

Papa Francis ambaye hakuonyesha kustushwa na tukio hilo, alimuacha motto huyo aketi, na kisha alipochoka, alisimama na kuenda kumghasi ghasi papa, ambaye alionyesha moyo wa ‘ubabu’ na kutomfanya chochote mtoto huyo.

Kama ambavyo waliagizwa, wazazi walikuja na wajukuu zao katika mojawapo ya mafundisho ya Papa Francis ambayo alikuwa akiyatoa kwa umati mkubwa, kuhusu jukumu la mababu na mabibi (grandparents).

Tukio la kuketi kwenye kiti hicho, kulimfanya kwa muda Fulani papa atabasamu wakati akiendelea na mafundisho, na wala hakujali hata pale motto huyo aliposhuka na kumshika mguu kama vile anamsumbua kwa kung’ang’ania kitu.

Hakika wazazi wa motto huyo wanaweza kuota ndoto kutokana na mtoto wao kufanya tukio hilo, na pengine ndoto mojawapo ni kuwa huyu ni mtumishi wa Mungu wa siku zijazo, maana ameshajua mahala panapomhusu, kwahiyo kinachosubiriwa ni kauli fupi tu, "Habemus Papam"

Papa akiendelea kufundisha huku mtoto nae akiendelea kuchezacheza madhabahuni. Picha kwa hisani ya L'Osservatore Romano kupitia AP.
Papa akiwa amemuwekea mkono mtoto ambaye jina lake halikufahamika mara moja baada ya kupanda madhabahuni. Picha kwa hisani ya L'Osservatore Romano kupitia AP.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment