Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, July 4, 2019

Frank Lampard asaini mkataba wa miaka mitatu Chelsea

Klabu ya Chelsea imemtangaza Frank Lampard kuwa kocha wake mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuionoa klabu hiyo. 

 Lampard

Lampard, 41, anaondoka katika klabu anayoinoa kwa sasa Derby County kuchukua hatamu katika klabu ya Chelsea ambayo alikuwa ni mchezaji kinara kwa miaka 13.
Anarithi nafasi iliyoachwa wazi na Maurizio Sarri, ambaye ameondoka mwezi uliopita kwenda kujiunga na miamba ya Italia klabu ya Juventus.

Lampard ameiwakilisha Chelsea katika mechi 648 Chelsea, na kunyakua mataji 11 na timu hiyo.
Hata hivyo anaenda kuingoza Chelsea katika kipindi ambacho wamepigwa marufuku ya kufanya usajili katika madirisha mawili na chombo kinachosiamamia mchezo huo FIFA, lakini tayari wameshakata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa masuala ya michezo.
 Lampard
"Ninafuraha isiyo kifani kurejea Chelsea kama kocha mkuu," amesema Lampard.
"Kila mtu anajua mapenzi yangu kwa klabu hii na historia yangu hapa. Lakini, malengo yangu kwa sasa ni juu ya kazi hii mpya na kujipanga kwa msimu ujao."
"Nipo hapa kufanya kazi kwa bidii, na natamani kazi ianze mara moja."
Uteuzi wa Lampard unakuja siku tisa tangu klabu ya Derby ilipomruhusu kufanya mazungumzo na Chelsea. na siku 18 toka Sarri alipoondoka klabuni hapo.
Lampard anakuwa kocha wa 10 kuifundisha Chelsea toka klabu hiyo iliponunuliwa na Roman Abramovich 2003.
Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia amesema Lampard amedhihirisha uwezo wake kwa kuiongoza Derby kukaribia kupanda Ligi ya Primia.
"Ni moja kati ya makocha vijana wenye uwezo mkubwa kwa sasa," amesema na kuongeza, "Inatupa faraja kubwa kumkaribisha tena Chelsea. Frank anaijua vyema klabu hii.
Lampard ameondoka Derby na makocha wasaidizi wake wawili, Jody Morris na Chris Jones. Petr Cech ambaye alikuwa ni kipa wakati Lampard akiwa kiungo Chelsea ataungana nao akiwa kama Mkurugenzi wa Ufundi.

Safari ya Lampard Chelsea

Embedded video
Lampard alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya West Ham kwa dau la pauni milioni 11 mwaka 2001.
Ameshinda taji la Klabu Bingwa Ulaya, Ligi ya Europa, na mataji matatu ya Primia, makombe manne ya FA na mawili ya Ligi.
Chelsea walichukua taji lao la kwanza la Primia kwa miaka 50 msimu wa 2004-05 na Lampard alifunga magoli 13 katika msimu huo, ikiwemo magoli yote katika ushindi wa 2-0 ambao ndio uliipa Chelsea ubingwa.
Akiwa na magoli 211 Lampard ndiye kinara wa magoli wa muda wote kwenye klabu ya Chelsea.
Lampard aliondoka Stamford Bridge ambapo ndiyo maskani ya Chelsea mwaka 2014.
Kwanza alienda Manchester City kwa muda mfupi ambapo alicheza mechi 32 na kufunga magoli sita.
Baada ya hapo akajiunga na New York City ya Marekani na kucheza mchezo wake wa kwanza Augosti 2015.
Alitangaza kustaafu baada ya miaka 21 ya kusakata kandada mwaka 2017.
Lampard amechezea timu ya taifa ya England michezo 106 na kufunga magoli 29.

BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment