Writen by
sadataley
12:13 PM
-
0
Comments
Rais
wa Tanzania, John Magufuli amewapongeza wananchi Chato mkoani Geita kwa
kuitikia wito wa Serikali ya Tanzania kuongeza kwenye uzalishaji mali,
hatua iliyochangia wilaya hiyo kupiga hatua za maendeleo.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai Mosi, 2019 na Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa imesema Rais
Magufuli ametoa pongezi hizo wakati akiwasalimia wananchi hao katika
eneo la Njiapanda, muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa
Chato akitokea Dar es Salaam.
Katika taarifa hiyo, imeeleza kuwa akiwa angani Rais Magufuli
amefurahishwa kuona namna wananchi wa Chato walivyochangamka kimaendeleo
kwa kujenga nyumba za kuishi za kisasa, majengo ya biashara, majengo ya
huduma za jamii na mashamba ya mazao mbalimbali.
“Nawapongeza wakazi wa Chato, mnachapa kazi kwelikweli na maendeleo
yanaonekana. Chato inabadilika, nilishasema asiyefanya kazi na asile,
tuendelee kushikamana,” amesema Rais Magufuli.
Mbali na hilo, Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea
kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa, kushikamana na kutobaguana ili
kulijenga Taifa kwa pamoja.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Magufuli yupo katika Kijiji cha Mlimani wilayani Chato kwa ajili ya mapumziko.
chanzo:ccm blog
No comments
Post a Comment