Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Monday, April 23, 2018

Mke wa mwana wa mfalme wa Uingereza amejifungua mtoto wa kiume

Mwana wa mfalme amepata mtoto wa tatu wa kiume

Haki miliki ya pichaPA
Image captionMwana wa mfalme amepata mtoto wa tatu wa kiume
Mtoto huyo ambaye atakuwa kitukuu wa sita wa malkia, amezaliwa katika hospitali ya St.Mary iliyopo Lindo Wing huko mjini London .
Hali ya afya ya mama na mtoto inaendelea vizuri .
William na CatherineHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWilliam na Catherine wapata mtoto mpya
Ujio wa mtoto wa tatu wa mwana wa Mfalme na mke wake Catherine amezaliwa saa saa saba majira ya Afrika mashariki.
Ukoo wa Malkia wa Uingereza
Image captionUkoo wa Malkia wa Uingereza
Familia zote wamepata taarifa ya ujio wa mtoto huyo na wanafuraha kwa habari hizo njema.
Mpaka sasa jina la mtoto mpya bado alijatangazwa.
Waandishi wa habari wakiwa nje ya hospitaliHaki miliki ya pichaPA
Image captionWaandishi wa habari wakiwa nje ya hospitali
Taarifa kutoka makazi ya malkia zinasema William alikuepo wakati mtoto huyo akizaliwa na majina anayoyapenda kwenye vitabu ni pamoja na Arthur, Albert, Frederick, James na Philip.
Swali ni je,mwana huyu mpya wa mfalme anaweza kuwa mfalme ajaye?Haki miliki ya pichaPA
Image captionSwali ni je,mwana huyu mpya wa mfalme anaweza kuwa mfalme ajaye?
Salamu za pongezi zimetumwa kutoka kwa waziri mkuu wa nchi hiyo Bi.Theresia May na anawatakiwa furaha na maisha mema yajayo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment