Writen by
sadataley
8:34 AM
-
0
Comments
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili mjini Berlin kwa mazungumzo na kansela Angela Merkel yenye lengo la kupata kuungwa mkono na kansela wa Ujerumani katika mipango yake ya mageuzi katika Umoja wa Ulaya, EU.
Kansela wa Ujerumani amesema kwamba licha ya kuwapo kwa tofauti baina ya nchi yake na Ufaransa katika maeneo machache ya pendekezo la maguezi ya EU, pande hizo mbili zitaweza kufanya kazi kupata muafaka ifikapo katikati ya mwaka huu.
"Tunahitaji kuwa na mjadala wa wazi na hatimaye kupata uwezekano wa kupata muafaka", Merkel amesema mjini Berlin leo wakati wa ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Ni muhimu kujibu maswali muhimu ya wananchi wa Ulaya kuhusiana na changamoto za dunia, alisema wakati akijadili mapendekezo ya Macron kwa ajili ya mageuzi katika Umoja wa Ulaya.
Merkel amesema Ulaya inaweza tu kutatua matatizo yake kwa pamoja, amedokeza kuhusu sera ya uhamiaji ya Umoja huo, mtazamo wa pamoja katika sera za mambo ya kigeni na kuendeleza zaidi uchumi wa eneo la sarafu ya euro pamoja na umoja wa sarafu kama maeneo ambayo yeye pamoja na Macron bado hawajakubaliana.
Kansela wa Ujerumani ana imani kwamba Umoja wa Ulaya utafanikiwa kupata matokeo mazuri katika maeneo mkubwa ya mageuzi, amesema hayo kabla ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo, akielezea matumaini juu ya kukamilisha umoja wa benki.
Mshikamano katika kanda ya euro
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kwamba mataifa wanachama wa Umoja wa sarafu ya euro yanapaswa kuongeza utaratibu wa mshikamano kama vile umoja wa benki katika mfumo uliopo hivi sasa kwa lengo la kuimarisha ushindani iwapo mataifa hayo yatataka kundi hilo la mataifa kuneemeka.
Kabla ya kuanza mazungumzo yao, viongozi hao walisema watawasilisha msimamo wa pamoja mwezi Juni katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya kuhusiana na mageuzi ya kanda ya euro yenye wanachama 19, ambapo Merkel alisema wamekubaliana lakini bado hakuna uhakika wa kutosha kwamba hakutakuwa na mzozo.
"Nimefurahi kwamba Emmanuel Macron amekubali mwaliko wangu. Kwa sababu huu ni mradi wa Ulaya na ni mradi ambao tunataka kuonesha kwamba sisi ni sehemu ya dunia na tunataka kufanya mageuzi na kuupa sura utandawazi. Na hiki ni kitu ambacho kinatuunganisha Ufaransa na Ujerumani."
Mkutano wa viongozi hao wawili unafanyika katika mazingira ya manung'uniko ya wabunge wa kundi la vyama vya kihadihina vinavyoongozwa na Merkel , ambao wanashaka kwamba wito wa Macron wa mshikamano zaidi katika kanda ya euro unaweza kushuhudia fedha za walipa kodi wa Ujerumani zikitumika kugharamia mataifa wanachama wenye matatizo.
Mtazamo wa Macron ni pamoja na kubadilisha mfuko uliopo hivi sasa barani Ulaya wa uokozi wa uchumi kuwa kama mfuko wa fedha wa Ulaya EMF , na kuwa kama kizuwizi katika mizozo wa hapo baadaye ya kifedha katika mataifa hayo, ambayo karibu yaparaganyike wakati wa mzozo wa madeni mwaka 2009.
Mwandishi: Sekione Kitojo

No comments
Post a Comment