Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, April 6, 2018

Kesi ya Jacob Zuma yapigwa kalenda


Kesi ya rushwa inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma imehairishwa mpaka Juni 8, 2018, itakaposomwa tena.

Jacob Zuma alifika mahakama kuu ya Durban leo asubuhi kusikiliza kesi yake ambayo ina mashtaka 16, yakiwemo ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji wa fedha.

Wafuasi wa Zuma walijikusanya maeneo ya karibu ya mahakama hiyo huku wakiimba nyimbo za kumsifu, wakisema hawatamuacha mpaka mwisho, na wengine wakikikesha kumuombea.

Kesi hiyo dhidi ya Zuma ilishwahi kufunguliwa na kusikilizwa, kisha kufutwa mwaka 2009, lakini sasa imeanza kusikilizwa tena baada ya kuondolwa madarakani, huku Rais aliyechukua wadhifa huo Cyril Ramaphosa akiahidi kukomesha vitendo vya rushwa nchini humo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment