Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Saturday, April 21, 2018

Burundi yapitisha sheria ya kukagua makazi ya watu bila kibali maalum.

Pierre Nkurunziza

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionPierre Nkurunziza
Bunge nchini Burundi limepitisha muswada wa sheria uliyowasilishwa na Waziri wa Sheria, kuruhusu polisi kufanya ukaguzi katika makazi ya watu bila kibali maalum.
Hatua hiyo imekosolewa vikali na wapinzani na watetezi wa haki za binaamu nchini humo.
Mwandishi wa BBC, Ismail Misigaro anaeleza kuwa muswada huo umepitishwa na sauti 97 na kupingwa na sauti 22 za wabunge wa upande wa upinzani.
Waziri wa Sheria Aimé Laurentine Kanyana aliutetea muswada huo kwa kile alichokitaja kuwa Burundi unakabiliwa na visa vya mauaji ya kikatili,ugaidi, baishara ya binadamu na kumiliki silaha kinyume cha sheria, utumiaji wa dawa za kulevya na hata ubakaji.
Hata hivyo,msako wa mchana hautohitaji kibali maalum,vikosi vya usalama vitaweza kuendesha msako wakati wowote.
Lakini, msako wa usiku utahitaji kibali maalum cha Kamishna wa polisi au idara nyingine husika.
Vyama vya upinzani nchini humo, vimehofia utaratibu huo, ambapo mkuu wa chama cha upinzani ,UPRONA , Abel Gashatsi ameelezea, 'Nchi yetu imetoka katika vita,lazima watu waogope.Muswada unaruhusu watu,kusakwa majumbani usiku, au kuwekewa kamera za uchunguzi za polisi. Ni hatari."
"Maafisa wa polisi na sheria lazima wawe na nidhamu,isije watu wakaleta silaha nyumbani kwao usiku.Halafu baadae akashtakiwa kwa kosa la kumiliki silaha" amesema Gashatsi.
Kwa upande wa chama kikongwe cha upinzani, FRODEBU wanasema muswada huo unakiuka katiba na kupendekeza baraza la Seneti kuurejesha na kuipinga.
Licha ya malalamiko hayo, muswada huo unasubiri hatua mbili : kuthibitishwa na baraza la Seneti na baadae kutiwa saini na Rais wa Burundi.
Kuna uwezekano mkubwa wa muswada huo kutopata pingamizi lolote bungeni, kwa sababu ya idadi kubwa ya wajumbe wa chama tawala cha CDD-FDD.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment