Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 1, 2018

Kibadeni aendelea kusisitiza Simba ina nafasi kubwa kubeba Ubingwa


Nyota wa zamani wa Simba na Tanzania, Abdallah Kibadeni ameendelea kusisitiza kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa kama wenyewe hawatavurugana.

Kibadeni ambaye anashikiria rekodi ya mchezaji pekee kufunga mabao matatu au hat trick katika mechi ya watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba, amesema Simba ndiyo wenye uwamuzi wa kuchukua au kutochukua.

“Nafasi waliyonayo ni kubwa snaa, timu yao iko vizuri na ni suala la wao tu kuendelea kupambana. Nafikiri hakuna wa kuwazuia Simba kuchukua ubingwa hasa kama wasipogombana wenyewe,” alisema, Pamoja na kuichezea, Kibadeni amewahi kuinoa Simba kwa nyakati tofautitofauti.

Baada ya mechi 19, Simba wanaongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 45 na wanafuatiwa na watani wao wa jadi Yanga wenye pointi 40.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment