Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, March 1, 2018

Hope Hicks: Mshauri wa Trump na Mkurugenzi wa mawasiliano ajiuzulu

White House Communications Director Hope Hicks leaves the US Capitol after attending the House Intelligence Committee closed door meeting in Washington, February 27, 2018

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBi Hicks amekuwa mmoja wa washsauri wakaribu wa Rais Trump
Mkurugenzi wa mawasiliano na mmoja wa mashauri wa karibu wa Rais Trump wa muda mrefu ameachia ngazi yake,mamlaka imesema.
Anaripotiwa kuwaambia wafanyakzai wenzake kuwa amehisi ametimiza wajibu wake katika ikulu ya White House.
Yeye ni mtu wa nne aliyeshika nyadhifa wa mkurugenzi wa mawasiliano.
Msemaji wa White House Sarah Sanders amesema haijulikani ni lini haswa Bi Hicks ataondoka.
Amekanusha kuwa hatua hio inahusiana na ushahidi amabyo Bi Hicks aliutoa mbele ya kamati Congress wakati aliporipotiwa kukiri kusema uongo wa wazi kwa niaba ya Bw Trump.
Wakati wa kampeni za uchaguzi, Bi Hick alifanya kazi kama khatibu wa mawasiliano. Alichukua nafasi wa kuungoza idara ya mawasiliano ya White House Agosti iliopita, baada ya ufutaji kazi wa ghafla wa
Bw Anthony Scaramucci.
Kabla yake , Sean Spicer na Mike Dubke walishika nyadhifa hio.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment