Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Wednesday, February 28, 2018

Mwimbaji Misri afungwa kwa kuikashifu mto Nile

Sherine ni mwanamuziki maarufu nchini Misri

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionSherine ni mwanamuziki maarufu nchini Misri
Mwimbaji wa Misri Sherine Abdel Wahab amehukumiwa miezi sita gerezani kwa kutania juu ya hali ya usafi wa mto Nile.
Sherine, ni mmoja wa waimbaji maarufu nchini humo pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice- alimwambia mashabiki wake kuwa kunywa maji kutoka mto huo kunaweza kumpatia vijidudu.
"Kunywa Evian badala yake." akatania
Mwimbaji mwingine, Laila Amer, pia alihukumiwa siku ya Jummane kifungo cha miaka miwili kutokana na video ya muziki.
Bi Amer - ambaye hana umaarufu kama Sherine - alipatwa na hatia ya 'kuchochea ufitini na uovu". Muongozaji wa kipindi na muigizaji walihukumiwa kwa vipindi vifupi.
Sherine, amehukumiwa na mahakama moja Cairo kwa kusambaza habari zisizo za kweli. Chombo cha habari Misri, Ahram kimesema aliagizwa kulipa paundi 5,000 za Misri.
Mzaha
Mashtaka dhidi ya Sherine yalifunguliwa mwezi Novemba, baada ya kuonekana video mtandaoni ikimuonesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya mto Nile?).akajibu ''Nikinywa maji ya mto Nile nitapata kichocho''. Kichocho ni ugonjwa unaojitokeza maeneo ya vijijini nchini Misri.
Mbali na kesi dhidi yake, Chama cha wanamuziki nchini humo kimetangaza kuwa kimempiga maruguku kuuimba wimbo huo kuhusu Misri.
Abdel Wahab baadae aliomba radhi kutokana na tukio hilo akiwa kwenye tamasha lililofanyika huko Jumuia ya falme za kiarabu zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Another singer, Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu
Mwanamuziki Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovuHaki miliki ya pichaSHYMA
Image captionMwanamuziki Shyma alihukumiwa kwa kucheza video ya maadili mabovu
Maamuzi ya mahakama yaliyotolewa siku ya Jumanne inafanya idadi ya wanamuziki kuhukumiwa kifungo kufikia watatu miezi ya hivi karibuni
Mwezi Desemba, Shaimaa Ahmed ajulikanaye kifupi Shyma alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kuonekana kwenye Video ya muziki akiwa amevalia nguo za ndani huku akila ndizi kwa mbwembwe.
alikutwa na hatia ya kuweka video yenye maadili mabaya akahukumiwa sambamba na muongozaji wa video hiyo.Baadae hukumu ilipunguzwa na kuwa ya mwaka mmoja baada ya kukata rufaa.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment