Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Sunday, February 25, 2018

Mkuu wa majeshi ya Korea Kaskazini azuru Korea Kusini

South Koreans protest against Gen Kim Yong-chol's visit in Paju, South Korea. Photo: 25 February 2018

Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionWaandamanaji wa Korea Kusini waliandamana kupinga ziara hiyo
Ujumbe wa Korea Kaskazini unaoongozwa na jenerali wa jeshi mwenye utata umevuka na kuingia Korea Kusini kwa sherehe za kufungwa mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi huko Pyeongchang.
Jenerali Kim Yong-chol analaumiwa kwa kuzamisha meli ya vita ya Korea Kusini mwaka 2010 ambapo wanajeshi 46 waliuawa. Korea Kaskazini inakana kuhusika.
Familia za waathiriwa na wabunge kadhaa wa Korea Kusini walifanya maandamano wakijaribu kuzuia ziara hiyo kwenye mpaka.
Gen Kim Yong-chol (centre) arrives in Paju, South Korea. Photo: 25 February 2018Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionGen Kim (katikati) anatarajiwa kukutana na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in
Ziara hiyo inafanyika wakati kuna kuboreka kwa uhusiano kati ya Korea hizo mbili.
Wakati wa mashindano ya olimpiki Korea Kaskazini na Kusini walitembea pamoja chini ya bendera moja wakati wa sherehe za ufunguzi na baadaye wakawa na kikosi cha pamoja na wanawake wa timu ya magongo.
Hata hivyo wataalamu wanaonya kuwa yanayofanaika sasa hayamalizi kikomo misukosuko ya kieneo hasa kufuatia majaribio ya nyuklia na ya makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini.
The South Korean naval corvette Cheonan is raisedHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAnalaumiwa kwa kuizamisha meli ya Korea Kusini
Ujumbe wa Marekani kwenye mashindano hayo unaojumuisha binti wa rais Donald Trump Ivanka, umekana kukutana na maafisa wa Korea Kaskazini.
Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza awamu mpya ya vikwazo dhidi ya korea Kaskazini.
Rasi ya Korea imegawanyika tangu vita vya miaka 1950 na pande zote mbili hazijawai kuwa na makubaliano ya mkataba wowote.
BBC
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment