Latest News

GNM Cargo

GNM Cargo
GNM CARGO & LOGISTICS

menu

Monday, June 12, 2017

Imetolewa tahadhari homa ya uti wa mgongo

SERIKALI wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa imetoa tahadhari kwa wakazi wa wilaya hiyo kutokana na kuwapo kwa mlipuko unaodhaniwa kuwa ni homa ya  uti wa mgongo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Khalfan Haule, alitoa tahadhari hiyo jana akisema kuwa tayari kumeripotiwa  kuwapo kwa homa inayodhaniwa kuwa ni ya ugonjwa wa uti wa mgongo kwenye kijiji cha Tentula na Kianda Kata ya Ikozi Sumbawanga Vijijini na kuwa mpaka sasa watu watatu wameugua na mmoja kufariki dunia kwa ugonjwa  huo.

Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Emmanuel Mtika, alisema ametuma timu ya wataalamu wa afya ili wafanye uchunguzi wa taarifa hizo katika vijiji hivyo.

Alisema kwa upande wa wagonjwa waliolazwa nao wanaendelea na matibabu, lakini vipimo havijatolewa ili kuthibitisha, lakini alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari katika kuepuka ugonjwa huo pamoja na magonjwa mengine.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment