Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Friday, January 20, 2017

Imepakiwa mnamo Hotuba ya Trump: 'Hili ni taifa lenu' Kutoka siku hii ya leo itakuwa Marekani kwanza ,Marekani Kwanza

Trump: Uwe mweupe au mweusi sote ni watu wamoja

Donald Trump akitoa hotuba baada ya kuapishwa
BBC
Donald Trump akitoa hotuba baada ya kuapishwa

'Watu wangu',  ahsanteni.
Pamoja tutashauriana kuhusu njia tutakayopeleka Marekani na dunia kwa miaka mingi ijayo.
Trump: "Hii ni siku yenu ,hii ni sherehe yenu na hii ni Marekani taifa lenu.Watu waliosahaulika na wanawake hawatasahaulika tena.kila mtu anakusikiza sasa.
Cha muhimu leo sio chama kinachodhibiti serikali.lakini iwapo taifa letu linadhibitiwa na watu.
Tunahamisha mamlaka kutoka Washington na kuwapatia nyinyi Wamarekani.
Washington iliimarika lakini watau hawakugawana utajiri wake.

'Uwe mweusi, mweupe ama udhurungi sote hutokwa na damu nyenkundu' 

"Tutaunganisha ulimwengu dhidi ya ugaidi ,ambao tutauangamiza kabisa duniani.

"Ni lazima tufikiri sana na kuwa na ndoto kubwa.
 Sitakubali wanasiasa amba huzungumza sana bila kuwatendea . 
 Wakati wa mazungumzo matupu umekwisha ,masaa ya kufanya vitendo yamewadia.
 Usikubali mtu akwambia kwamba haiwezi kufanyika''.

Trump ameahidi kwamba  kazi na elimu zitapatiwa kipau mbele katika utawala wake.
"Tumeyafanya mataifa maengine kuwa tajiri,dhabiti .Moja baada ya nyengine viwanda vyetu vimeondoka 
Kutoka siku hii ya leo itakuwa Marekani  kwanza ,Marekani Kwanza

Pamoja, tutaifanya Marekani kuwa taifa kuu tena. Tutaifanya kuwa taifa tajiri tena. Ijionee fahari tena, tutaifanya salama tena. Na ndio, pamoja, tutaifanya Amerika kuwa taifa kuu tena.

Trump anapoendelea kuhutubu, tayari ukurasa wa rais wa Marekani kwenye Twitter umebadilishwa na kuwa wake. Ujumbe ulioandikwa na utawala wa Obama umefichwa na kuhifadhiwa.


« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment