Latest News

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)

UNIVERSITY OF IRINGA (Formerly Tumaini University-Iringa)
CALL FOR MARCH INTAKE APPLICATION 2017/18
NOW OPEN!
DEADLINE 30/03/2018
CALL 0743 802 615, 0677 048 677Read More

menu

Thursday, January 19, 2017

Jengo kubwa laporomoka Iran na kuua wengi

Hakuna kilichobaki wakati jengo hilo la ghorofa 17 lilipoporomoka

Haki miliki ya pichaEPA
Image captionHakuna kilichobaki wakati jengo hilo la ghorofa 17 lilipoporomoka

Wazima moto wengi wanahofiwa kuaga dunia baada ya jengo moja kubwa kwenye mji mkuu wa Iran Tehran, kushika moto na kuporomoka.
Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofga 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporoka kwa kwa sekunde chache

Jengo hilo lilikuwa ghorofa la kwanza refu mjini TehranHaki miliki ya pichaTASNIM NEWS AGENCY/REUTERS
Image captionJengo hilo lilikuwa ghorofa la kwanza refu mjini Tehran

Zaidi ya watu 200 pia nao waliripotiwa kujeruhiwa kwenye mkasa huo.
Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.
Moto huo unaripotiwa kuanza mwendo wa saa 04:30 GMT siku ya Alhamisi, wakati watu hawakuwa bado wameingia.

Wazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadhaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadha

Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.
Kituo kimoja cha runinga cha serikali kilinukuu afisa mmoja akisema kuwa kati ya watu 50 na 100 wanaaminiwa kukwama chini ya vifusi.

Waokoaji walifanikiwa kuwaokoa baadhi ya wazima motoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWaokoaji walifanikiwa kuwaokoa baadhi ya wazima moto
Baadhi ya wale waliosurika waliangua kilioHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBaadhi ya wale waliosurika waliangua kilio
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment