Writen by
sadataley
3:14 PM
-
0
Comments
IDADI ya vifo vya ajali ya basi la kampuni Vitu laini lenye namba za usajili T910 linalofanya safari zake kati ya Lulanzi wilaya ya Kilolo na Iringa mjini kufeli breki na kuligonga lori lenye namba T724 AVV scania lililobeba Mbao jana eneo la Tagamenda Iringa mjini imeongezeka kufikia watu wawili baada majeruhi mmoja Neema Fungo (37) mkazi wa Ndiwili Iringa kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu . .
Mtandao huu wa matukiodaimaBlog umefika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na kuzungumza na uongozi wa Hospitali hiyo leo
Muunguzi mfawidhi msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Victoria Ntara alisema walipokea majeruhi 52 wa ajali hiyo iliyotokea eneo la Tagamenda katika barabara kuu ya Iringa – Kilolo mmoja kati ya majeruhi alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na majeruhi hao wengi wao walitibiwa na kuondoka na hadi sasa ni 20 ndio ambao wamebaki wakiwemo wanaume 11 na wanawake 9 huku majeruhi watatu hali zao ni mbaya na wapo katika uangalizi wa karibu
Jana Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi kati ya majeruhi hao yupo dereva ambaye pia ni mmiliki wa basi la vitu laini John Upete (49) ambae ameumia usoni na mguuni nahali yake inaendelea vizuri
Wakati dereva wa lori Fadhil Mbanga (25) yeye alitoka salama huku mzee Lupyana Mtenga (70) ambae alikuwa amekaa siti ya mbele akipoteza maisha kwenye ajali hiyo .
Chanzo:Mtandao wa Godwin Francis
No comments
Post a Comment